Instagram story viewer> @secyrose> Post
2 days ago
Co Creator: cwhrdstz tamwa_ endfemicidetz_
Mwezi wa tisa na wa kumi tumepoteza wanawake wengi kwa sababu ya ukatili. Aibu kwetu sote!

Tumepoteza binadamu. Tumepoteza maisha yenye ndoto, matumaini na mustakabali. Tumeshindwa kuwalinda wanawake na kuhakikisha wanakuwa salama katika jamii zetu.

Ni wakati wa kuacha ukimya, kuacha kuhalalisha ukatili na kuchukua hatua za kweli. Wanawake wanastahili kuishi, si kuishi kwa hofu.

Leo tunapaza sauti na kusema:

TUMECHUKIZWA!
TUNA HUZUNI!
TUNADAI HAKI NA USALAMA WETU!

Hatutaki kuendelea kuomboleza wanawake ambao wangeweza kuwa hai leo. Tunataka hatua, uwajibikaji, haki na mifumo inayolinda maisha ya wanawake.

Usalama wa wanawake si jukumu la wanawake pekee. Ni wajibu wetu sote.

SHAME ON US! TUMECHUKUA MUDA MREFU SANA KUSHUGHULIKIA UKATILI HUU.

#EndFemicideTz
#notofemicidetz 
#KomeshaMauajiYaWanawakeTz
1
Posted On: November 1st 2026, 12:07 pm

Comments (1)
stuarthilda 4 hours ago

stuarthilda

Its paining.. Watu wameannza ku normalise mauaji kwa kisingizio wivu wamapenzi. Hakuna mtu anaehaki ya kukatisha uhai wa mwenzie. Wasichana na wanawake ukiona dalili za mauaji, sogea pembeni mpishe na hasira zake, itakusaidia baada ya muda.

More posts

back to up