Instagram story viewer> @pharm_solomon> Posts
146.1K
followers
1702
following
π‘¨π’‘π’π’•π’‰π’†π’„π’‚π’“π’š πŸ’‰
POSTS STORIES REELS TAGGED
πŸ˜„πŸ˜„ Hebu kichafueni tu , Repost , Share , kila kitu  na mimi niwe na Post 1 yenye maajabu πŸ”₯❀️

#pharmsolomom by @pharm_solomon
22k
5 days ago
Download
Kujipost kidogo 😁 kisha tutaendelea

#pharmsolomon by @pharm_solomon
603
3 years ago
Download
Tumebeba hiyoooooooooo πŸ˜‚πŸ˜‚ Mje sasa tufurahi pamoja ❀️ wote mlionipigia kura mje hapa , mmetisha sana jamani asanteni sana πŸ™πŸ™

Kwanza kabisa nitoe shukrani zangu za dhati kabisa kwenu followers wangu na watu wote mnaonifuatilia , asanteni kunipa ushindi na tuzo hii ni yetu sote.

Mwaka jana mlifanya yenu tukabeba Tuzo , mwaka huu pia mkaona bado nawafaa sana , asanteni sana πŸ™ . Lakini nipende pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa dada @dinamarious kwa kutambua mchango wa vijana na watu mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii hasa Instagram katika kuelimisha jamii , kutoa huduma bora n.k Binafsi nashukuru sana

Kutokana na dharura sikuweza kwenda ila nilituma muwakilishi wa kupokea tuzo yetu πŸ† . Next time Mungu akipenda tupate tuzo nyingine na Uzima ukiwepo ntajitahidi kuhudhuria

Asanteni sana πŸ™ nawapenda sana

#pharmsolomon by @pharm_solomon
679
2 years ago
Download
Hizi ni baadhi ya picha za Wasomali zilizopigwa mwaka 1890 , na zinapatikana katika Album moja yenye picha 50 . Zipo katika Maktaba Kuu ya Taifa la  Ufaransa (BibliotheΜ€que nationale de France , BnF), Idara ya Jeografia inayoitwa Département Société de Géographie

πŸ‡ΈπŸ‡΄ Katika kipindi cha ukoloni, maeneo ya Wasomali yaligawanywa chini ya utawala wa Waingereza, Waitaliano, Wafaransa na Waethiopia. Mgawanyo huu uliwatenganisha Wasomali katika maeneo tofauti yaliyotokana na mipaka ya kikoloni.

Licha ya kutawaliwa na wageni, Wasomali waliendelea kuhifadhi utambulisho wao wa kitamaduni, mila, desturi na lugha yao tajiri. Wakati huohuo, harakati mbalimbali za upinzani, zikiwemo harakati za Dervish, zilipambana dhidi ya utawala wa kikoloni.

#pharmsolomon by @pharm_solomon
7
11 hours ago
Download
Hili wengi hawalifahamu πŸ€”

Ikitokea ukaona mwanaume alikua pacha na kisha mwenza au Mke wake akazaa watoto mapacha basi ujue huyo mwanamke ndio anahusika hapo na sio Mwanaume. Kwa sababu ili mapacha watokee ni lazima mwanamke atoe mayai zaidi ya moja na yote yarutubishwe au atoe yai moja ambalo likirutubishwa litagawanyika mara mbili kutoa mapacha ( Ule ugawanyikaji wa yai hausababishwi na mbegu za mwanaume ✍️)

Kwahiyo mbegu za mwanaume zinabaki kwenye swala la kurubisha yai au mayai , basi. Na mbegu hazina mchango mwingine wowote kwa swala hili la mapacha ( Iwe wanaofanana au Wasiofanana )
.
.
πŸ“š Mwanamke yeyote nje na swala la historia ya familia yake ( Upande wa mama,bibi mzaa mama n.k ) anaweza kupata mapacha ( Inatokea na sio lazima iwe kwa historia tu), hii inatokea tu kawaida kama bahati. Na njia nyingine ni ile ya maabara IVF
.
.
.
πŸ”Š SHARE POST HII 

#pharmsolomon by @pharm_solomon
52
2 days ago
Download
WHO wanashauri usubiri angalau miezi 6 , lakini mashirika mengine kama vile ACOG, NIH, na RCOG wenyewe wanasema miezi 3 inatosha na hakuna utofauti wowote kati ya kusubiri sana na kubeba mimba nyingine mapema ikiwa sababu za mimba kuharibika zitapatiwa suluhisho , hii ni kulingana na tafiti zao walizofanya

Lakini pia wameendelea na kusema , mwanamke abebe mimba nyingine pale anapohisi kwamba yupo tayari kimwili na kiakili pia
.
.
⛰️ Kama mimba itaharibika ikiwa na zaidi ya wiki 20 , mwanamke anashauriwa kusubiri angalau miezi 6-12 kabla hajabeba ujauzito mwingine
.
.
πŸ”ˆ Kabla hujabeba ujauzito mwingine baada ya mimba kuharibika nakushauri jitahidi ufahamu angalau kidogo tu kwanini iliharibika , na ikiwa kuna namna yoyote ya kukusaidia kabla hujabeba mimba nyingine , hii itasaidia ujauzito ujao uwe na asilimia kubwa ya kuendelea vizuri bila kuwepo madhara yaliyotokea kwenye ujauzito uliopita . Itapunguza madhara au kuyamaliza kabisa , naamini hakuna kitu kinauma kama mimba kuharibika , sio tu madhara ya kimwili bali hata kiakili athari ni kubwa na inaleta msongo wa mawazo hasa kwa mwanamke au wazazi wanaotamani kupata mtoto
.
.
Kama kuna mtu alikumbana na hii changamoto na bado hajapata suluhisho anitafute DM ✍️
.
.

#pharmsolomon by @pharm_solomon
4
13 hours ago
Download
Hii inaitwa Free and Fair Election πŸ˜‚πŸ˜‚ by @pharm_solomon
20
13 hours ago
Download
Tupo na mwingine , anaitwa @prisca__lyimo QUEEN OF THE YEAR : MISS COSMO INTERNATIONAL 2026 πŸŒŸπŸ‘‘

Twendeni tukawashe moto πŸ”₯ kama kawaida yetu , maelekezo ni yale yale 😁 , New Followers ina mchango mkubwa wa Point 70 βœ…, Kwahiyo yale mafekero yote niliyowafundisha kuyafungua mkayatumie huku , mkachafue hali ya hewa
.
.
πŸ”Š NAMNA YA KU VOTE :
.
.
Njia ya 1:

Ingia kwenye hii account @missosology_queens itafute picha ya Prisca , utaiona kama hiyo niliyoipost . Ukifika pale angalia juu kulia au chini kushoto , utaona Follow button , iguse , hapo utakua counted as New Follower ✍️ 
Ukimaliza sasa , anza kulike , repost , save halafu mwaga comments za kutosha kama mvua .
.
.
Njia ya 2:

Nenda kwenye insta stories yangu , utakuta post ya Mshiriki wetu moja kwa moja . Ukifika iguse itafunguka , kama kawaida angalia kulia juu au chini kushoto , utaona Follow button , iguse , hapo utakua counted as New Follower ✍️ 
Ukimaliza sasa , anza kulike , repost , save halafu mwaga comments za kutosha kama mvua 
.
.
.
Voting points zipo hivi πŸ‘‡πŸ‘‡

πŸ””Follow β€” 70 points
πŸ””Like ❀️ β€” 5 points
πŸ”” Comment πŸ’¬ β€” 5 points
πŸ””Share πŸ”„ β€” 5 points
πŸ””Save πŸ”– β€” 5 points

Hatupotezi muda , tuondoke wataalamu wa hizi kazi πŸ«‘πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

#pharmsolomon by @pharm_solomon
156
14 hours ago
Download
Wahusika si mpo ? Basi muwe mnafanyiwa massage kidogo inasaidia πŸ€”

Hii inasababishwa na hormones za uzazi pale viwango vinapokua juu , lakini pia husababishwa na uzalishwaji wa prostaglandins kwa wingi , kwahiyo badala ya kufanya kazi kwenye tumbo la uzazi tu kusaidia mikazo ili tishu za kuta za mji wa uzazi zitoke kama hedhi ( Tishu + damu ) madhara yake hutokea na kwenye misuli mingine ya jirani hasa misuli ya makalioni

Maumivu unayopata ni kama vile ulifanya mazoezi ya makalio au miguu (Mfano squatting πŸ‹οΈ) au

Maumivu yakiwa makali sana unaweza tumia paracetamol, ibuprofen au ukapata massage kidogo itasaidia

.
.
.
πŸ”Š SHARE / TAG NA WENGINE WAJIFUNZE PIA πŸ’‘ by @pharm_solomon
10
14 hours ago
Download
Haya sasa Kesho mapema sana 10:30 AM JNIA  mkampokee Miss wetu @jihandimack πŸ€”πŸ˜ Si mlimpa Ushindi wenyewe , haijaisha mpaka Kesho 

Mlipambana sana na 95% , respect kwenu watu wa kazi πŸ«‘πŸ‘

#pharmsolomom by @pharm_solomon
9
15 hours ago
Download
Wale wapenzi wa kula maini mpo ? πŸ‘‚ Kuna jambo lenu hapa ✍️
.
.

Kula maini kwa wingi sana kunaweza kuwa na madhara :
.
.
πŸͺ½ Sumu ya Vitamini A
.
Ini lina kiwango kikubwa cha vitamini A. Kula kwa wingi sana kunaweza kusababisha mwili kuwa na kiwango kikubwa cha vitamin  A, hali inayoweza kusababisha kichefuchefu, kizunguzungu, maumivu ya kichwa, na katika kwa matumizi makubwa na ya muda mrefu inaweza  kuharibu ini, nywele kukatika ovyo , maumivu ya mifupa n.k
.
.
πŸͺ½ Kiasi Kikubwa cha Shaba
.
Ini lina shaba kwa kiwango kikubwa pia. Kula kwa kiasi kikubwa kunaweza kusababisha sumu ya shaba, ambayo inaweza kusababisha  matatizo mengine ya kiafya kama vile matatizo ya tumbo , ini kupata madhara , matatizo ya akili ( Mood kubadilika ) n.k .
.
.
πŸͺ½ Kiwango Kikubwa cha Cholesterol
.
Ini lina cholesterol nyingi, ambayo inaweza kuwa tatizo kwa watu wenye magonjwa ya moyo, ingawa uhusiano kati ya cholesterol kwenye mlo na magonjwa ya moyo unatofautiana kwa kila mtu.
.
.
.
πŸ“š Wataalamu wa lishe wanashauri kwamba watu wale maini kwa kiasi ,  Kula maini mara moja kwa wiki (Ukizidiwa sana basi isizidi mara 2 kwa wiki)  ni salama na itakupa virutubisho muhimu bila madhara

Kuhusu kula maini, kiasi kinachopendekezwa ni gramu 100 hadi 150 kwa mlo mmoja ( Mfano sasa ukiweka maini yaliyopikwa kwenye kikombe chenye ujazo wa robo lita , yatafikia kama robo tatu ya kikombe au kuzidi nusu kikombe kidogo , hii ninewaelezea ili upate picha ni kama kiasi gani kwa mlo mmoja ) , kwa maini ya kuku unaweza tumia hadi gram 200 kwa sababu hayana Vitamin A nyingi sana ukilinganisha na maini ya Wanyama kama Ng'ombe / mbuzi nk . Kiasi hiki kwa kawaida ni salama na hukupa virutubisho muhimu bila kuhatarisha sumu ya vitamini A au matatizo mengine yanayoweza kutokana na kula ini kwa wingi.

Kwa watu wengi, kula maini mara moja kwa wiki kwa kiasi hiki kinatosha kupata faida za kiafya bila kuzidisha. Kumbuka kiasi ni jambo la kuzingatia 🀝 . Wale ambao wao kila siku au wanaruka siku moja au mbili wanakula maini hii sio salama sana , changamoto nyingi za kiafya tunazopitia huanzia kwenye lishe 
.
.
.
πŸ”Š SHARE / TAG βœ…

#pharmsolomon by @pharm_solomon
4
18 hours ago
Download
We mwenyewe unashangaa hili joto ndo lianze siku hizi ? πŸ˜‚

#pharmsolomom by @pharm_solomon
11
a day ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up