Instagram story viewer> @pointfmtz> Posts
1768
posts
22.1K
followers
58
following
πŸ†„πŸ…ΊπŸ†„πŸ†πŸ…°πŸ†‚πŸ…° πŸ†πŸ…°πŸ†‚πŸ…ΌπŸ…Έ πŸ††πŸ…° @pointfmtz
πŸ“» π—§π—”π—‘π—šπ—” | 𝗗𝗒𝗗𝗒𝗠𝗔 | π—¦π—œπ—‘π—šπ—œπ——π—” | π—œπ—₯π—œπ—‘π—šπ—” |
#π‘’π‘™π‘–π‘šπ‘€π‘’π‘›π‘”π‘’π‘€π‘Žπ‘π‘’π‘Ÿπ‘’π‘‘π‘Žπ‘›π‘– πŸ”Š 96.5
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Kata ya Ipagala Jijini Dodoma, Insp. Nungwana amewataka wananchi kuongeza umakini katika masuala ya kiulinzi majumbani kwao hasa wakati wanapotoka kwenda katika majukumu yao."Dodoma yasasa sio kama ya miaka nane iliyopita, tujitahidi kuimarisha usalama majumbani mwetu ili kuepukana na wizi unaoepukika" Alieleza Kamanda huyo wakati akisalimu Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ipagala Jijini Dodoma siku ya leo.Mbali na hayo Kamanda huyo aliambatana na Watu wa Dawati la jinsia kutoka Kanda ya Tanga, Dar Es Salaam na Dodoma ambao wamewaasa wananchi kupiga Vita ukatili sambamba na kujitokeza kwa wingi katika Madawati ya Kijinsia ili wapate suruhisho la migogoro mbalimbali inayowakabiri na sio kujichukulia sheria mkononi.__________________________________πŸ“» Ikumbatie Point Fm 96.5 popote wakati wote.πŸ”Š Tunasikika online kupitia Radiobox na Radiogarden #Pointfm #ulimwenguwaburudani by @pointfmtz
0
8 hours ago
Download
HII NDIO WEEKEND YA KUFOSI? πŸ˜‚ by @pointfmtz
2
2 days ago
Download
Itazame makala ya baadhi ya Wachezaji Waliosajiliwa na kutambulishwa mpaka sasa nchini Tanzania.🎀 @magingoepifania✍️ @j19michezo _______________________________πŸ“» Ikumbatie Point Fm 96.5 popote wakati wote🌎 Online tufuate kupitia Radiobox na Radiogarden by @pointfmtz
0
2 days ago
Download
Yooh!! Talk Of the Town iko hewani, Saa nane hadi kumi jioni, Mkali wa sauti zinazokita vizuri kwenye Bongo Hip Hop @majesty__tz anasikika akizungumzia safari ya Muziki wake, Changamoto, Mafanikio na mchakato wa kuandika KITABU. Ikumbatie Point Fm 96.5 MHz upatane na @mwinjanavil@robby_the_dj mpaka mwisho wa Show. by @pointfmtz
6
2 days ago
Download
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesemakutokubaliana kati ya Serikali na Watetezi wa Haki zaBinadamu katika baadhi ya masuala si ugomvi waladhambi, bali ni sehemu ya kawaida ya jamii yakidemokrasia.Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati waMkutano Mkuu wa Wanachama wa Mtandao waWatetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Nchimbiamesema uwepo wa mitazamo tofauti unasaidia kujenga mijadala yenye tija na haupaswi kutafsiriwa kama uadui._____________________________________πŸ“» Ikumbatie Point Fm 96.5 wakati wote popoteπŸ”Š Online tupo Radiogarden na Radiobox πŸ™ Usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii by @pointfmtz
14
2 days ago
Download
Simba SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya baada ya kutangaza rasmi kumsajili mshambuliaji lbrahim Doumbia kutoka AS Korofina ya Mali kwa mkataba wa miaka miwili.Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 anatajwa kuwamshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufungamabao na kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi.Katika msimu uliopita akiwa na AS Korofina, Doumbiaalibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Mali baada yakufunga mabao 17 pamoja na kutoa pasi za mabao kwawenzake.Aidha, akiwa na timu ya taifa ya Mali chini ya miaka 20,amecheza mechi 26 na kufunga mabao 22, jambolinaloonyesha kiwango chake cha juu akiwa badonimchezaji kijana.Uongozi wa Simba umeeleza kuwa usajili wa Doumbia ni sehemu ya mkakati wa kuunda kikosi imarakitakachowania ubingwa wa mashindano ya ndanipamoja na kufanya vizuri kwenye Ligi ya MabingwaAfrika wakiongeza kuwa Mashabiki wa Simba sasa watakuwa na matumaini makubwa kuona mshambuliaji huyo akiongeza nguvu mpya kwenye safu ya ushambuliaji msimu ujao._______________________________________#Pointfm #ulimwenguwaburudani by @pointfmtz
0
2 days ago
Download
Rapa Mkongwe Kutoka Marekani Snoopdogg ametangaza Kuachia Filamu Yake Agosti 6 Mwaka Huu ambapo filamu hiyo itaangazia safari ya maisha ya Snoop Dogg kuanzia alipokulia katika mitaa ya Long Beach, California, jinsi alivyoingia kwenye muziki wa Hip Hop na kufanikiwa kuwa mmoja wa marapa wenye ushawishi mkubwa duniani. Pia itaonesha changamoto alizopitia katika maisha na kazi yake ya muziki, mafanikio yake katika biashara na burudani, pamoja na mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki kwa zaidi ya miongo mitatu.Kitu gani unakingoja kwenye filamu ya Mkali huyu?______________________________________πŸ“» Ikumbatie Point Fm wakati wote popote.🌎 Online tupo Radiogarden na Radiobox #Pointfm #ulimwenguwaburudani by @pointfmtz
0
2 days ago
Download
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amesema Serikaliinatekeleza mradi wa kupeleka minara ya kurahisishahuduma za mawasiliano katika maeneo tisa ya Wilaya ya Mpwapwa yenye changamoto hiyo ambapo mpaka sasa tayari imepeleka minara 57 kwenye Kata 28 ambayo imesaidia kutatua changamoto hiyo.Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mlembule, Wilaya ya Mpwapwa katika viwanja vya shule ya msingi Mlembule wakati wa ziara yake ya kikazi iliyokwenda sambamba na ukaguzi wa miradi ya maendeleo Julai 23, 2026, Waziri Kairukialisema;"Kwa upande wa Wilaya ya Mpwapwa, tayari tumekwishaleta minara takribani57 na mna mawasiliano takribani Kata 28, zimebakia Kata 5, vile vile, tuna mradi ambao tunautekeleza wa takribani shilingi Bilioni 1.6 ambao Dodoma tutaleta minara 14, lakini pia kwa upande wa Wilaya ya Mpwapwa, kuna Kata ya Ipera kvwenye Kijiji cha Kikuyu, kata ya Masa katika Kiji cha Mkoleko na kwenyewe pia tutahakikisha tunaleta minara".Aidha, aliongeza kuwa, Serikali inafanya jitihada hizokwa kuwa huduma za mawasiliano kwa sasa si anasabali ni vya lazima kutokana na kutumika katika kila sekta.__________________________________#Pointfm96.5 #ulimwenguwaburudani by @pointfmtz
0
2 days ago
Download
Karibu ufuatilie Habari kwa Ufupi siku ya leo Julai,24 kutoka hapa @Pointfmtz 96.5, Msomaji ni @happyangelbalisidya πŸ“Ή @ciphaleetza__________________________________πŸ“» #Pointfm #ulimwenguwaburudani by @pointfmtz
3
2 days ago
Download
Watu 23 wakiwemo viongozi na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka moja la kushiriki kwenye mikutano ya kigaidi.Watuhumiwa hao walisomewa shtaka hilo jana Julai 23, mwaka huu katika mahakama hiyo iliyopo kwenye Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Buswelu Wilaya ya lemela, Mwanza. Ambapo, wamefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi na kusomewa shtaka linalowakabili kwa nyakati tofauti na kwa makundi kulingana na maeneo wanakodaiwa kutenda makosa hayo, katika Kesi Namba 16375 ya mwaka 2026 na 16377 ya mwaka 2026.Waliopandishwa kizimbani ni Alphaxad Nyamwaga (57), Fantson Mpango (49), Abely Mwesa (62), Hassan Said (43), Emmanuel Wambura (30), Adam ldd (23), Damas Sadock(31), Petrol Mabula (40), Abdul Kagwidi (28), Devid Mahendeka (20), Philipo Masatu (31), Edward Mikindo (28) na Emmanuel Doto (26).Wengine ni Deus Masalago (41), Mohamed Tosha (37), Fabian Nguvumali (52), Samwel Mtani (45), Samwel Kobell (40), Julius Makonga (34), Fanuel Lutana (35), Philipo Kulwa (37), Philipo Shipuluko (50) na Hamis Mnyivua (35).Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai 4, na Julai 7 mwaka huu, katika wilaya za Nyamagana na llemela mkoani humo.Akisoma shtaka hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Mwanza, Erick Marley amesema shtaka linalowakabili washtakivwa 13 kutoka Wilaya ya llemela ni kutenda kosa la kushiriki kwenye mikutano ya kigaidi.Upande wa mashtaka uliongozwa na Wakili mkuu wa Serikali na mkuu wa mashtaka mkoa wa Mwanza, Joseph Maugo akisaidiana na wakili wa serikali mwandamizi Janess Kihwelo, na mawakili wakili wa serikali, Sileo Muzullah na Evance Kaiza.Akisoma maelezo ya shtaka hilo, Wakili Maugo amesema washtakiwa hao walitenda makosa hayo kinyume na kifungu cha 4(1)(2)(a), 5(a) na 12(1)(c) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi, Sura ya 19 Toleo la 2023, ikisomwa pamoja na aya ya 24 ya Katiba na vifungu vya 57(1) vya Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Kiuchumi na Uhalifu Uliopangwa, Sura ya 200 Toleo la 2023._____________________#Pointfm #ulimwenguwaburudani by @pointfmtz
0
2 days ago
Download
Licha ya kuwa anaendelea kutumikia kifungo cha miaka 10 gerezani, Mkali wa Muziki, @tory lanez hajaacha kufanya muziki. Akiwa nyuma ya nondo ameendelea kurekodi, kutoa nyimbo na albamu mpya jambo linaloonyesha kuwa mazingira magumu si lazima yazime kipaji au ndoto ya mtu kwani Mkali huyo yuko jela kutokana na kesi yake ya kupatikana na hatia ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion mwaka 2020, kisha akahukumiwa kifungo cha miaka 10. Hata hivyo, bado anaendelea kukata rufaa huku akiendeleza kazi zake za muziki kutoka gerezani kwank hata hivi sasa anazungumziwa sana kutokana na miradi yake mipya kama LOL: Slutty Bass, From Prison, na Made You Think I Was Gone huku watu wengi wakishangazwa na uwezo wake wa kuendelea kuwa sehemu ya mjadala wa muziki duniani licha ya kuwa gerezani._________________________________πŸ“» Ikumbatie Point Fm wakati wote popote🌎 Online tusikilize kupitia Radiobox na Radiogarden #Pointfm #ulimwenguwaburudani by @pointfmtz
0
2 days ago
Download
Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa leo Julai 23, 2026imemuhukumu kifungo cha miaka thelathini (30) jela kwa kila kosa mtuhumiwa OMARIISSA CHIPUNGU (34),Mkulima wa kiji cha Mbekenyera Wilaya ya Ruangwa,aliyekutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya ainaya Bangi pamoja na mbegu zake.Inaelezwa kuwa, mnamo tarehe 08/05/2026 katika Kijijicha Mbekenyera, Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi,mtuhumiwa alikamatwa akiwa na Bangi zenye uzito wa kilogramu 32.24017 na mbegu za Bhangi zenye uzito wa gramu 780 na kisha kufikishwa mahakamani tarehe 09 Juni 2026 na kusomewa mashitaka yake yalikuwayanamkabili.Katika kesi hiyo, mtuhumiwa alikiri makosa yote mawilimbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mhe. Jonas Lyakundina Mwendesha Mashtaka wa Serikali John Remmy, huku kukiri kwake kukipelekea mahakama kumtia hatiani bila shaka.Mahakama ilibainisha kuwa makosa ya kusafirisha nakumiliki dawa za kulevya ni hatari kwa jamii na yanamadhara makubwa kwa mustakabali wa vijana na Taifakwa ujumla. Hivyo, hukumu ya kifungo cha miakathelathini kwa kila kosa imetolewa ili iwe fundisho kwawengine na kuimarisha mapambano dhidi ya biasharaharamu ya dawa za kulevya.____________________________πŸ“» Ikumbatie Point Fm wakati wote popote.🌎 Tufuate Online kupitia Radiobox na Radiogarden #Pointfm #ulimwenguwaburudani by @pointfmtz
0
2 days ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up