Instagram story viewer> @posta_news> Posts
21.4K
followers
21
following
Ukurasa Rasmi wa Shirika la Posta Tanzania | Posta Tupo Kivingine |
POSTS STORIES REELS TAGGED
📍 ARUSHA
🗓️ Oktoba 2026

♦️NAIBU WAZIRI AFUNGUA JUKWAA LA TANO LA EACO LA POSTA NA LOGISTIKIA♦️

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama, amefungua rasmi Jukwaa la Tano la EACO la Posta na Logistikia (EPLF 5), jijini Arusha, akisisitiza umuhimu wa teknolojia na ubunifu katika kuboresha huduma za posta na kukuza biashara za kidijitali Afrika Mashariki.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Naibu Waziri amesema sekta ya posta na logistikia ina nafasi muhimu katika kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, biashara za mtandaoni na kuwaunganisha wafanyabiashara na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya malipo, ufuatiliaji wa mizigo na anwani za makazi, ikiwemo Mfumo wa Taifa wa Anwani za Makazi (NaPA), ili kuongeza ufanisi wa huduma na kurahisisha biashara zinazovuka mipaka.

Sambamba na hayo, Naibu Waziri, ametembelea mabanda ya maonesho na kuhimiza nchi wanachama wa EACO kushiriki zaidi katika maonesho yajayo kwa kuwasilisha ubunifu na teknolojia zinazoweza kuchochea uwekezaji na maendeleo ya sekta hiyo.

Shirika la Posta Tanzania (TPC) ni miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika maandalizi na utekelezaji wa jukwaa hilo, kwa kushirikiana na EACO, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na wadau wengine.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania. by @posta_news
3
2 days ago
Download
📍 BERNE, USWISI
🗓️ Oktoba 2026

♦️TANZANIA YAWEKA HISTORIA, YATWAA TUZO YA NYOTA INAYONG’AA KATIKA MAENDELEO YA POSTA DUNIANI♦️

Tanzania imeweka historia katika sekta ya posta Duniani baada ya kutwaa tuzo ya Nyota Inayong’aa (Rising Star) ya mwaka 2026, inayotolewa na Umoja wa Posta Duniani (UPU) kwa nchi zilizofanya maboresho makubwa katika maendeleo ya huduma za posta.

Tuzo hiyo imetolewa kupitia Kiashiria Jumuishi cha Maendeleo ya Posta *Integrated Index for Postal Development – 2IPD), kilichotathmini maendeleo ya sekta ya posta katika nchi 181 Duniani.

Aidha katika tukio hilo, Tuzo hiyo imepokelewa na Mhe. Angellah Kairuki (Mb),Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  kwa niaba ya Tanzania, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Posta Duniani( UPU) Jijini Berne, Uswisi.

Utambuzi huu ni kutokana na juhudi za kuendeleza sekta ya posta kwa kuzingatia nguzo nne za Kielezo Jumuishi cha Maendeleo ya Posta (2IPD), ambazo ni uhakika wa huduma, umuhimu wa huduma na ustahimilivu.

Tuzo hii ina maana  kuwa kichocheo cha kuongeza bidii katika maeneo yote manne yaliyopimwa. Pia inaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa huduma za posta zinaendelea kuwa na umuhimu kama kichocheo cha ujumuishaji wa kidijitali, kifedha na kijamii, kama ambavyo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akisisitiza mara kwa mara.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania by @posta_news
2
7 days ago
Download
📍 MOSHI, KILIMANJARO
🗓️ Oktoba 2026

*SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LASHIRIKI TAMASHA LA KAHAWA 2026*

Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeendelea kuunga mkono juhudi za kukuza sekta ya kahawa nchini kwa kushiriki na kuwa miongoni mwa wadhamini wa Tamasha la Kahawa la saba (Kahawa Festival 2026) linalofanyika kuanzia Oktoba 8 hadi 10, 2026 katika Kampuni ya Tanganyika Coffee Curing Company Limited (TCCCo Ltd), mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Tamasha hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kahawa, wakiwemo wakulima, wachakataji, wafanyabiashara, wawekezaji na wataalamu, kwa lengo la kujadili fursa za kukuza uzalishaji, kuongeza thamani, kupanua masoko na kuimarisha ushindani wa kahawa ya Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa tamasha hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Hassan Omary Bomboko, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa ambaye amelipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa mageuzi makubwa linayoyatekeleza, hususani katika kupanua wigo wa huduma za usafirishaji. Aidha, amesema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za Shirika hilo katika kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Meneja wa Posta Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Abubakari Athumani, amewataka wananchi na wadau wa sekta ya kahawa kutumia huduma za usafirishaji zinazotolewa na Shirika la Posta kufikisha bidhaa zao kwa wateja ndani na nje ya nchi.

Aidha, amesema ushiriki wa Posta katika tamasha la (Kahawa Festival)unalenga kuwawezesha wakulima, wafanyabiashara na wajasiriamali kupata huduma za usafirishaji zinazowaunganisha na masoko mbalimbali, hivyo kuwasaidia kufikisha bidhaa zao kwa wateja kwa urahisi, usalama na ufanisi.

*Imetolewa na;*
*Kitengo Cha Mawasiliano ;*
*Shirika la Posta Tanzania .* by @posta_news
0
7 days ago
Download
📍 ARUSHA
🗓️ Oktoba 2026

♦️*TANZANIA YACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAKUU WA TAASISI ZA POSTA(EACO CEO'S POSTAL FORUM)*♦️

. Macrice Mbodo, Mwenyekiti mpya wa Jukwaa hilo

Tanzania imechaguliwa kuongoza Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Posta Afrika Mashariki( East Africa CEO's Postal Forum) kwa kipindi cha miaka mitatu, baada ya Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Macrice Mbodo, kuchaguliwa  na MA PMG wenzake kuwa Mwenyekiti wa jukwaa hilo.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi uliopo ndani ya Jengo la PAPU, jijini Arusha, chini ya makubaliano ya Wakuu wa Mashirika ya Posta kutoka nchi za Afrika Mashariki, waliokutana kujadili uanzishwaji wa jukwaa hili la uongozi na vipaumbele vya maendeleo ya sekta ya posta katika ukanda huo.

Kupitia nafasi hiyo, Tanzania itakuwa na fursa ya kuongoza uratibu wa vipaumbele vya maendeleo ya sekta ya posta kikanda, kuimarisha ushirikiano baina ya nchi wanachama na kusukuma mbele utekelezaji wa miradi ya pamoja inayolenga kuboresha huduma za posta na usafirishaji.

Aidha, kikao hicho kilijadili miradi inayopendekezwa na inayolenga kuunganisha mifumo ya biashara mtandao baina ya nchi za Afrika Mashariki, kuboresha vituo vya usafirishaji na usambazaji wa vifurushi, kuimarisha mifumo ya anwani za kidijitali na kusaidia mashirika ya posta kuimarisha matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma.

Katika kuendeleza maazimio hayo, wakuu hao walikubaliana kuanzisha Kamati ya Mageuzi ya Posta ya EACO (EACO Postal Transformation Committee), itakayoshughulikia maandalizi ya kina ya miradi, mipango ya utekelezaji, muda wa utekelezaji na mapendekezo ya ushirikiano pamoja na ufadhili.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania. by @posta_news
2
15 hours ago
Download
📌 Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) tunawatakia Watanzania wote heri ya kumbukizi ya miaka 27 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tunaenzi mchango wake katika kujenga umoja na amani kwa maendeleo ya Taifa letu.

#WorldPostDay 
#OnePostalNetwork #InfinitePossibilities #WorldPostDay2026 
#PostaTanzania by @posta_news
1
3 days ago
Download
🏆🏆🏆🏆🏆🏆🏆🏆🏆🏆🏆

📌 TUNAPIGA KAZI. TUNALETA MATOKEO. TUNANG’ARA KIMATAIFA.

#WorldPostDay 
#OnePostalNetwork #InfinitePossibilities #WorldPostDay2026 
#PostaTanzania by @posta_news
1
4 days ago
Download
📍 *KILIMANJARO*
🗓️ Oktoba 2026

♦️BODI YA KAHAWA YATAMBUA MCHANGO WA POSTA KATIKA USAFIRISHAJI, YATOA TUZO YA UBINGWA♦️

Shirika la Posta Tanzania limepata tuzo ya kutambuliwa kama mdau muhimu wa usafirishaji katika Sekta ya Kahawa. Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) katika Tamasha la Kahawa (Kahawa Festival 2026), lililofanyika kuanzia Oktoba 8 hadi 10, 2026, katika viwanja vya Tanganyika Coffee Curing Company Limited (TCCCo Ltd), mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa kufunga tamasha hilo, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini, Mhe. Godfrey Eliakimu Mnzava, amewapongeza waandaaji, wadhamini na washiriki katika tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya kahawa na uchumi wa nchi.

Aidha, amewahimiza wadau kuendelea kushirikiana katika kuboresha uzalishaji, kuongeza thamani ya kahawa na kupanua masoko ya ndani na nje ya nchi, huku akisisitiza umuhimu wa kutumia huduma za usafirishaji na mifumo ya biashara inayowezesha bidhaa kuwafikia wateja kwa wakati.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Michael Mwanachuo, amesema ushiriki wa Shirika la Posta katika tamasha hilo ni sehemu ya juhudi za kutangaza huduma zake za usafirishaji na kuwafikia wadau mbalimbali. Ameeleza kuwa Posta inaendelea kutoa fursa kwa wakulima na wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao na kuzifikisha katika masoko ya ndani na nje ya nchi kupitia huduma zake za usafirishaji.

Naye, Meneja wa Posta Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Abubakari Athumani, amesema tuzo hiyo ni chachu kwa Shirika la Posta kuendelea kutoa huduma bora za usafirishaji na usambazaji wa bidhaa kwa wakulima, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta ya kahawa.

Kahawa Festival ni jukwaa muhimu la kuunganisha wadau wa sekta ya kahawa, kutangaza ubora wa bidhaa hiyo ya Tanzania na kukuza fursa za biashara, uwekezaji na masoko kwa manufaa ya wakulima na wafanyabiashara.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania. by @posta_news
0
5 days ago
Download
📍 MOSHI, KILIMANJARO
🗓️ Oktoba, 2026

Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Michael Mwanachuo, pamoja na Meneja wa Posta Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Abubakari Athumani, wakitumia Siku ya Posta Duniani na tamasha la Kahawa (Kahawa Festival) kuzungumzia fursa zinazopatikana kupitia huduma za Posta kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali kupitia Redio Galaxy (Galaxy Fm).

#WorldPostDay
#One Postal Network
#Infinite Possibilities
#WorldPostDay2026
#PostaTanzania

@upu_un 
@wizara_mawasiliano_ict_tz
@tcra_tanzania 
@angellah_kairuki
@maelezonews by @posta_news
1
7 days ago
Download
📍 DAR ES SALAAM
🗓️ 09 October, 2026

♦️ SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAPOKEA MAGARI KUTOKA UMOJA WA POSTA DUNIANI (UPU)♦️

Shirika la Posta Tanzania (TPC) limepokea magari yaliyotolewa na Mfuko wa ubora  wa Huduma (QSF) kutoka Umoja wa Posta Duniani (UPU)  kwa lengo la kuimarisha usafirishaji na kuongeza ufanisi wa huduma za posta nchini.

Makabidhiano hayo yalifanyika Posta House jijini Dar es Salaam ambapo Mjumbe wa Bodi ya Umoja wa Posta Duniani (UPU), Eng. Clarence Ichwekeleza, alikabidhi magari hayo kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Ferdinand Kabyemela, kwa niaba ya Postamasta Mkuu, Bw. Daniel Macrice Mbodo, kabla ya kuyakabidhi kwa Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Mshanga

Magari hayo ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uwezo wa Posta kuwahudumia wananchi na wafanyabiashara kwa ufanisi zaidi, sambamba na juhudi za kuboresha huduma za usafirishaji wa mizigo na vifurushi nchini. 

#WorldPostDay
#OnePostalNetwork
#InfinitePossibilities
#WorldPostDay2026
#PostaTanzania

@upu_un
@wizara_mawasiliano_ict_tz
@tcra_tanzania
@angellah_kairuki
@maelezonews by @posta_news
4
7 days ago
Download
♦️ SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAADHIMISHA SIKU YA POSTA DUNIANI 2026 ♦️

Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha Siku ya Posta Duniani leo, tarehe 9 Oktoba 2026, maadhimisho hayo yamefanyika katika Hoteli ya King Jada, Morocco, jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Sweetbert Mkama, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Nicolous Merinyo Mkapa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), pamoja na Bw. Ferdinand Kabyemela, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Posta Tanzania kwa niaba ya Postamasta Mkuu, wafanyakazi wa Shirika hilo, viongozi wa Wizara, TCRA, kampuni za usafirishaji, pamoja na wadau mbalimbali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri amelipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa juhudi zake katika kuboresha utoaji wa huduma za posta. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kutumia Mfumo wa Ufuatiliaji wa Mizigo na Vifurushi (CMS) katika usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi ili kuongeza ufanisi na uhakika wa huduma.

Vilevile, alihimiza ushirikiano kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, TCRA, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Shirika la Posta Tanzania katika kuimarisha ubora wa huduma na matumizi ya mfumo wa CMS.

Kwa upande wake, Bw. Ferdinand Kabyemela aliwashukuru wadau kwa ushirikiano wao na kusisitiza kuwa huduma za Posta ni salama, za uhakika na za haraka, huku akihimiza wananchi na wafanyabiashara kuendelea kuzitumia.

Hafla hiyo pia imehusisha utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano ya uandishi wa barua pamoja na kutambua kampuni za usafirishaji zilizofanya vizuri katika matumizi ya mfumo wa CMS, ambapo Shirika la Posta Tanzania limeibuka mshindi wa nafasi ya kwanza.

Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani yanaendelea kuonesha nafasi muhimu ya huduma za posta katika kuunganisha watu, kuwezesha biashara na kurahisisha usafirishaji wa mizigo na vifurushi, huku teknolojia ikiendelea kufungua fursa zaidi za utoaji wa huduma.

#WorldPostDay
#OnePostalNetwork
#InfinitePossibilities
#WorldPostDay2026
#PostaTanzania by @posta_news
0
7 days ago
Download
SERIKALI YAWATAKA WASAFIRISHAJI KUUNGANISHA MIFUMO YA UFUATILIAJI WA VIFURUSHI.

Na Mwandishi Wetu - WMTH, Dar es Salaam.

Serikali imewataka watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na huduma za haraka kujisajili na kuunganisha mifumo yao na mifumo ya kitaifa ya ufuatiliaji na ubadilishanaji wa taarifa, ili kuwawezesha wateja kufahamu mahali nyaraka na vifurushi vyao vilipo katika kila hatua ya safari.

Wito huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb) wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani 2026. Amesema mifumo ya ufuatiliaji wa vifurushi (Tracking and Tracing) ni muhimu katika kuimarisha uwazi, usalama na ufanisi wa huduma za posta nchini.

Dkt. Mkama amewahimiza watoa huduma ambao bado hawajaunganisha mifumo yao kufanya hivyo, akieleza kuwa ushirikiano na ubadilishanaji wa taarifa ni msingi wa kujenga mtandao jumuishi wa posta unaotoa huduma bora kwa wananchi na wafanyabiashara, huku ukilinda faragha na taarifa za wateja.

Aidha, amezipongeza kampuni za usafirishaji wa haraka zilizoanza kuunganisha mifumo yao na Mfumo wa Ufuatiliaji wa Mawasiliano (Communication Monitoring System – CMS) unaosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya wadau kutumia teknolojia kuboresha huduma za posta.

Ameeleza kuwa sekta ya posta inaendelea kubadilika kutokana na ukuaji wa biashara mtandao na ongezeko la mahitaji ya huduma za haraka, salama, nafuu na zinazofikika. Ameongeza kuwa mifumo iliyounganishwa itasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kufikia masoko mapya, kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mkama amelitaka Shirika la Posta Tanzania pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuandaa Wiki ya Posta kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani mwaka 2027 kwa ukubwa, ili kutoa fursa kwa kuelimisha umma kwa Wananchi wengi zaidi kuhusu huduma za posta na mchango wake katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. taken in Dar es Salaam, Tanzania by @posta_news
0
8 days ago
Download
🗓️ 9 Oktoba 2026

♦️ HERI YA SIKU YA POSTA DUNIANI 2026♦️

Shirika la Posta Tanzania (TPC) linaungana na wadau wa Posta duniani kuadhimisha Siku ya Posta Duniani, kaulimbiu ikiwa ni Mtandao mmoja wa Posta, Fursa zisizo na kikomo *“One Postal Network, Infinite Possibilities.”*

Kaulimbiu hii inaonesha umuhimu wa mtandao mmoja wa posta katika kuunganisha watu, biashara na jamii kupitia fursa mbalimbali za huduma za posta.

#WorldPostDay
#One Postal Network
#Infinite Possibilities
#WorldPostDay2026
#PostaTanzania

@upu_un 
@wizara_mawasiliano_ict_tz 
@tcra_tanzania 
@angellah_kairuki 
@maelezonews by @posta_news
2
8 days ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up