Instagram story viewer> @score.shayo> Posts
66
followers
316
following
ScoreShayo/Breaking News | Transfers | Results
POSTS STORIES REELS TAGGED
Kocha Ibenge, amekaza msuli kwa wapinzani wao ZED FC baada ya mchezo wao kupata sare ya 1-1 huku Azam FC wakiwa ugenini, kibarua kigumu bado kwa Ibenge, anahitaji ashinde kwa bao 1, pekee kupitia mchezo wao wa marudiano wa CAFCC dhidi ya ZED FC. Mchezo wa CAFCC, raundi ya pili, unatarajiwa kuchezwa uwanja wa Azam Complex, utaamua hatima ya Azam FC kuelekea kwenye hatua ya makundi au kutolewa.
#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
2 minutes ago
Download
Kiungo wa klabu ya Barcelona, Frenkie de Jong, ameitwa kwenye kikosi cha kwanza ambacho kocha Hansi Flick ameona ni muda sasa wa kumpa nafasi, baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha na kipindi cha kupona.

“Ni mchezaji bora sana, bora sana, na tunafurahi sana kuwa naye hapa,” amesema kocha Hansi Flick, ambaye pia amesisitiza kuwa mchezaji huyo atapangiwa dakika za kucheza kwa uangalifu.
.#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
3 hours ago
Download
Klabu ya 15 De Agosto imekumbwa na changamoto ya usafiri inayoweza kuchelewesha kuwasili kwake nchini Tanzania kwa ajili ya mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Simba SC.

Taarifa zinaeleza kuwa CAF imeusogeza mbele mchezo huo kwa siku moja kufuatia changamoto zilizoripotiwa na klabu hiyo.

Mchezo huo uliokuwa umepangwa kuchezwa Oktoba 20, 2026, sasa unatarajiwa kuchezwa Jumatano, Oktoba 21, 2026.

Mabadiliko hayo yanatoa muda zaidi kwa timu hiyo kukamilisha safari yake na maandalizi ya mchezo huo muhimu wa kimataifa. .#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
3 hours ago
Download
Mchezaji kutoka klabu ya Bayern, Harry Kane, amekubali kuongeza mkataba na klabu yake.

Taarifa kutoka ndani ya Bayern zinadaiwa kuwa mchezaji huyo pamoja na viongozi wa klabu wameafikiana juu ya uwepo wake tena. Mazungumzo baina ya mchezaji na klabu yako mwishoni, huku kisibitisho cha makubaliano hayo kikiwa ni kwa njia ya mdomo pekee.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anaendelea kung’ara akiwa katika kiwango bora kabisa, akifunga mabao 50 katika mwaka huu na kuonekana miongoni mwa vinara wa kuwania tuzo ya Ballon d’Or. .#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
5 hours ago
Download
Parc des Princes unaenda kuweka historia ya mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa Jumanne, ambao ni PSG dhidi ya Barcelona.

Inaelezwa kuwa kupitia mchezo huo, PSG imelazimika kuuza tiketi za mchezo huo kwa bei ghali kwa mashabiki wake. Tiketi moja inachukuliwa kwa gharama isiyopungua €1,300 kwa kila tiketi.

Mfumo wa uuzaji tiketi umeboreshwa kulingana na uwanja huo kujaa mashabiki wa klabu yao PSG.

€500 ndiyo bei ya chini kwa viti vilivyo sehemu za juu za uwanja.

€810–€850 kwa viti vya safu za mbele.

Hadi €1,300 kwa viti vilivyo karibu na njia ya wachezaji kuingia uwanjani!

Mmiliki mmoja wa tiketi ya msimu aliuza kiti chake kwa €800, lakini mnunuzi aliishia kulipa €948 baada ya kuongezwa gharama za huduma!
.#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
a day ago
Download
PSG wana mpango mkubwa wa kumsajili beki Eric García kutoka Barcelona.

PSG wamelenga kutoa ada isiyopungua €70 milioni kwa ajili ya kumsajili beki huyo. Matamanio ya klabu hiyo ni kuona benchi lao la ufundi likipata mlinda mlango sahihi ili kuipa mafanikio PSG. .#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
a day ago
Download
kwa upande wangu lakini naona kuna uwezekano mkubwa wa Feisal kuhamia Young Africans, sio kwa upendo ila kulingana na pesa watakazotoa pindi atakapomaliza mkataba wake na Azam FC.

Fei ana mpango wa kuondoka Azam FC kwa makubaliano ya pande zote mbili. Mchezaji huyo kwa sasa amebakiza miezi 7, maana ataondoka Azam mnamo mwezi wa 12,

klabu yoyote inaweza kumchukua kama mazungumzo yatakwenda sawa na mchezaji huyo ila asilimia kubwa Yanga SC wanaweza kufanya kitu juu ya mchezaji huyo.

Yanga SC wanaweza kutoa pesa yoyote ili kumpata Fei, na uwezekano huo upo wazi endapo hauna asilimia zote. .#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
a day ago
Download
Rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji, maarufu kama Mo, ametimiza ahadi yake ya kutoa bonasi ya Tsh milioni 500 kwa wachezaji wa Simba SC kufuatia ushindi walioupata katika mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Young Africans.

Hatua hiyo inakuja baada ya Simba SC kuibuka na ushindi katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, huku ahadi ya Mo Dewji ikiwa sehemu ya motisha aliyokuwa amewawekea wachezaji kabla ya pambano hilo.

Malipo hayo ni habari kubwa kwa mashabiki wa Simba, ambao sasa wanaendelea kusherehekea ushindi huo pamoja na motisha iliyotolewa kwa kikosi chao.

Mo Dewji ameendelea kuhusishwa na motisha za kifedha kwa wachezaji wa Simba, hasa katika michezo mikubwa inayobeba uzito wa kihistoria kwa klabu hiyo. .#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
a day ago
Download
MANARA: YANGA INGEWEZA KUIFUNGA SIMBA HADI MABAO 5

Afisa Habari wa zamani wa Young Africans, Haji Manara, amezungumzia mchezo wa Kariakoo Derby uliochezwa Oktoba 10, akidai kuwa Yanga ilikuwa na uwezo wa kupata ushindi mnono dhidi ya Simba SC.

Manara amesema kuwa kama Yanga ingefanikiwa kupata mabao mawili mapema, huenda ingeendelea kuongeza mabao na kufunga hadi matano kutokana na uwezo wake wa kushambulia.

Ameeleza kuwa Yanga ina sifa ya kucheza kwa kasi na kujiamini inapokuwa kwenye mashambulizi, bila kujali mbinu ambazo wapinzani wake wanatumia. Hata hivyo, katika mchezo huo, Simba SC ndiyo iliyofanikiwa kupata matokeo mazuri.

Kwa upande mwingine, Manara anaamini kuwa tatizo la Yanga halipo kwenye uwezo wa wachezaji pekee, bali pia kwenye mbinu za kocha. Amesisitiza kuwa hilo halimaanishi kocha anapaswa kuondolewa, bali ni muhimu kuhakikisha anatumia mbinu zinazoweza kuendana na uwezo wa wachezaji alionao.
.#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
a day ago
Download
TANZANIA YAPATA UWAKILISHI CAFCL, KHALID ABDALLAH ATEULIWA NA CAF

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid Abdallah, ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa Kamishna wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya APR FC ya Rwanda na Zamalek SC ya Misri.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 16, 2026, katika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda, ukiwakutanisha miamba hiyo miwili ya soka la Afrika katika hatua ya mashindano hayo.

Uteuzi huo unamuweka Khalid Abdallah katika nafasi muhimu ya kusimamia masuala ya kiutawala yanayohusiana na mchezo huo kwa mujibu wa majukumu ya Kamishna wa mechi chini ya taratibu za CAF.

Kwa upande wa Tanzania, uteuzi huo ni nafasi ya mwakilishi kutoka TFF kushiriki katika usimamizi wa mashindano ya ngazi ya juu ya soka barani Afrika.

Macho ya mashabiki wa soka yataelekezwa Kigali, ambako APR FC na Zamalek SC zitakutana katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

.#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
a day ago
Download
Tetesi za usajili wa dirisha dogo zinaendelea kuhusishwa na klabu ya Simba SC, huku taarifa kutoka kwa wachambuzi zikidai kuwa klabu hiyo inapanga kufanya mabadiliko katika safu yake ya ushambuliaji kwa kumuondoa Doumbia, anayecheza nafasi ya namba 9.

Katika tetesi nyingine, mshambuliaji wa zamani wa Young Africans, Prince Dube, anatajwa kuwa na mpango wa kurejea Tanzania na kujiunga na wapinzani wao, Simba SC.

Taarifa hizo zinadai kuwa Yanga ilikuwa na nia ya kuendelea kuwa na huduma ya Dube na inadaiwa kumuwekea ofa kubwa, lakini mchezaji huyo anatajwa kuwa na wazo la kurejea Tanzania akiwa na lengo la kuitumikia Simba SC.

Hata hivyo, hadi sasa suala hilo bado ni tetesi za usajili, na hakuna uthibitisho rasmi kuhusu uwezekano wa Dube kujiunga na Simba SC.

Mashabiki wa Simba wanasubiri kuona kama tetesi hizo zitageuka kuwa usajili halisi katika dirisha dogo. Taarifa zaidi zitafuatia kadri hali itakavyoendelea. .#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
a day ago
Download
SIMBA SC YAPEWA NAFASI YA KUPIGANIA TIKETI YA HATUA INAYOFUATA DAR ES SALAAM

Klabu ya Simba SC imewapa taarifa mashabiki wake kuhusu michezo yake miwili ya hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya FC 15 de Agosto kutoka Equatorial Guinea, ambayo itachezwa jijini Dar es Salaam, Tanzania, katika Uwanja wa Uhuru.

Mabadiliko hayo yamethibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), baada ya timu hizo mbili kufikia makubaliano ya kucheza mechi zote mbili, ya nyumbani na ugenini, nchini Tanzania kutokana na Equatorial Guinea kukosa uwanja unaokidhi vigezo vinavyotakiwa.

Kwa upande wa Simba SC, sasa macho na nguvu vinaelekezwa kwenye michezo hiyo miwili, huku kikosi hicho kikilenga kupata ushindi katika mechi zote mbili ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.

Mchezo wa kwanza utapigwa Oktoba 20, 2026, saa 10:00 jioni, huku Simba SC ikiwa katika nafasi ya ugenini dhidi ya FC 15 de Agosto. Mchezo wa marudiano utachezwa Oktoba 25, 2026, saa 10:00 jioni, katika uwanja huo huo, safari hii Simba SC ikiwa mwenyeji.

Kwa upande wa benchi la ufundi, kocha Steve Barker anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho katika harakati za kutafuta matokeo mazuri, huku mashabiki wakisubiri kuona namna atakavyokitimiza kikosi chake katika michezo hiyo muhimu.

Pia, macho yanaweza kuelekezwa kwa rais wa Simba SC, Mohammed Dewji, ambaye huenda akatoa kauli au ujumbe maalumu kwa timu kabla au baada ya michezo hiyo. Simba imekuwa ikitumia motisha mbalimbali, ikiwemo zawadi za fedha na ahadi kwa wachezaji, katika maandalizi ya mashindano makubwa.

Kwa sasa, swali kubwa kwa mashabiki wa Simba ni kama kikosi hicho kitaweza kutumia vizuri nafasi ya kucheza mechi zote mbili nyumbani na kupata matokeo yatakayokipeleka hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika. .#Scoreshayoupdates by @score.shayo
0
a day ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up