instagram story viewer > #KATIBA

#KATIBA

Posts
Akizungumza katika kikao Kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Machi 2, 2026, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Dk Abdallah Possi amesema "Tanzania ni Taifa huru, na lina jukumu kuu la kulinda amani, kusimamia Katiba, na kuwalinda watu wake. Kulinda heshima ya mchakato wa uchaguzi sio chaguo, bali ni wajibu wetu kikatiba. Hatua zozote zilizochukuliwa kuzuia vurugu na kulinda amani zinapaswa kuonekana kama wajibu halali wa Serikali" #JamiiForums #JFMatukio #UchaguziOktoba29
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba amesema Serikali imepanga kuanza mchakato wa kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, kifungu cha 13, kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 15, katika mwaka wa fedha 2026/2027. Katimba amesema hayo leo Mei 13, 2026, Bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Taska Restituta Mbogo ambapo amesema “Sheria ya Ndoa wakati inatungwa mwaka 1971 ilitanguliwa na ukusanyaji wa maoni kwa jamii kwa njia ya White paper ambapo Watanzania wote walishirikishwa, Aidha tangu Sheria hii itungwe imeshafanyiwa marekebisho mara nne mwaka 1974, 1996 na mwaka 2006 mheshimiwa mwenyekiti maoni yalikusanywa kwenye mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, Arusha, Dodoma na Mara kuhusu sheria ya ndoa sura ya 29” “Hata hivyo baada ya uchambuzi wa maoni yaliyokusanywa imeonekana kuna hitaji la kukusanya maoni zaidi katika Mikoa iliyosalia zoezi ambalo limeapangwa kuanza katika mwaka wa fedha 2026/27 mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Seriakali itawasilisha muswada Bungeni ambao utakuwa umezingatia maoni ya Wananchi” #MillardAyoUPDATES
WATANZANIA TUSILALE KWENYE AJENDA YA KATIBA MPYA LEO Kupitia Kipindi Cha JANAnaLEO Cha @wasafifm SALUMU MWALIMU Aliyekuwa Mgombea Wa Kiti Cha Urais Wa CHAUMMA 2025 #JanaNaLeo With @adellatillya_backup & @edokumwembe & @oscaroscarjr & @hajismanara__ #JanaNaLeo #WasafiFM #MchezoUmebadilika
Bungeni: Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Happines Daniel Ngwando ameshauri kufanyiwa marekebisho kwa sheria ya mirathi kwani inawanyonya wanawake na kuwapendelea watoto, jambo ambalo huleta utata pale ambapo mme anakuwa na nyumba kubwa na ndogo Akichangia makadirio ya mapato na matumizi Bajeti ya wizara ya Katiba na Sheria, amesema haiwezekani mali ambazo mke amepambana akiwa na mmewe, kisha mirathi zinarithiwa na watoto kwa kupitia jina la Baba
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Juma Zuberi Homera akitambulisha Familia yake wakiwemo Wake zake wawili walioambatana na Watoto wake, leo Aprili 24,2026 Bungeni Jijini Dodoma, wakati akisoma hotuba ya uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo. #SAThabari #SATmediaupdates
KATIBA MPYA NI MALI YA WATANZANIA Cc. @salmadacotha @musakipanya @gerald_hando #MchezoUmebadilika #WasafiFm #GoodMorning
MURUA BALANCE FACE MIST: - ni tona ya kusawazisha, kukuza, kujenga na kung'arisha ngozi ili kuboresha mwonekano na kuweka rotuba (mbolea) katiba ngozi. -. MURUA CLEANSING OIL :-ni vipodozi vinavyofanya kazi ya kusafisha uso kwa kiasi kikubwa kabisa kwa kuyayusha na kuondoa kiasi kikubwa cha uchafu wa usoni kama vile mafuta, jasho, vumbi, seli zilizokufa na takataka zingine. Matokeo yake ni kwamba mtu ambaye ametumia kipodozi hiki anabaki na ngozi safi kabisa na inayong’aa kwa sababu kiasi kikubwa cha uchafu na vitu vingine vilivyokuwa vinafunika ngozi yake vimeondolewa. Ufanisi wake katika kusafisha uso ni mkubwa kuliko kitu kingine chochote..... UTAZIPATA HIZI ZOTE KWA 50,000/=ZOTE 2 CALL NOW 0752300068
MWAKA AMBAO SIASA ZA TANZANIA ZILISIMAMA! 🇹🇿🔥 Kuna kipindi kwenye historia ya nchi ya Tanzania, siasa haikuwa habari za kwenye TV tu, bali ilikuwa ni "muziki" uliokuwa unachezwa kila kona ya mtaa. Mwaka 2015, chini ya mwamvuli wa UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi), nchi ilishuhudia mshike mshike ambao nadhani (wahenga mtuweke sawa) haukuwahi kuonekana tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. Haikuwa tu kuhusu vyama kuungana (CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi, na NLD), bali ilikuwa ni lile "vibe" la mabadiliko lililoanzia barabarani hadi kwenye majukwaa. Lowassa alipoingia sasa, upepo ulibadilika ghafla! Kila mkutano ukawa kama tamasha, kila mtaa ukawa na wimbo mmoja tu "UKAWA". Nani anasahau watu kusafisha barabara kwa kupiga deki? Nani anasahau nyimbo za "Mabadiliko... Lowassa!" zilizovuma hadi vijijini? Ilikuwa ni kipindi ambacho kila kura ilionekana kuwa na thamani ya dhahabu, na hofu ya "nani atatoboa" ilitanda nchi nzima. Licha ya matokeo yaliyopatikana, UKAWA ya 2015 ilibaki kama alama (landmark) inayotukumbusha kuwa kuungana kunaweza na kutikisa kusimamisha nchi. Hebu rudisha kumbukumbu nyuma kidogo... Wewe mwaka ule ulikuwa wapi na unakumbuka tukio gani la kipekee ambalo hutakaa ulisahau kwenye ule uchaguzi? Tuambie kwenye comment hapa chini tuchat kidogo! 👇🗳️ 🎥 Credit: @globaltvonline & #teamlowassa - YouTube #followsaomediatz
Edwin Sifuna: Chama cha ODM iko na katiba yenye inasema tuitishe uchaguzi, James Orengo ajitangaze aseme anawania kiti cha party leader, tukutane na huyo Oburu. Mnanona nani atashinda? Orengo ama Oburu?
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, ametimiza ahadi yake ya kumaliza changamoto ya maji katika Shule ya Sekondari Nasuli kwa kukabidhi tanki la maji lenye uwezo wa lita 5,000 pamoja na pampu ya maji. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Jopo la Wawakilishi wa Mbunge jimboni humo, Mwalimu Saidi Homera, alisema kuwa pamoja na vifaa hivyo, Dkt. Homera tayari ameshawaleta wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti wa kuchimba kisima kirefu kitakachosaidia upatikanaji wa maji kwa uhakika. Aliongeza kuwa kisima hicho kinatarajiwa kuchimbwa hivi karibuni. Kwa nyakati tofauti, Mkuu wa shule hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule kwa niaba ya wazazi, pamoja na wanafunzi, walieleza furaha yao na kushukuru juhudi hizo, wakibainisha kuwa changamoto ya maji ilikuwa ikikwamisha maendeleo ya shule kwa kiasi kikubwa.
SERIKALI KUANZA NA MARIDHIANO, KATIBA MPYA #Habarikuu #HabarileoUPDATES #TumeyaChande
Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. @zainabkatimba, leo Aprili 27, 2026 Mkoani Morogoro amefungua kikao kazi cha uhakiki na uthibitishaji wa rasimu ya taarifa ya hali ya haki za binadamu kwa mzunguko wa nne wa Mfumo wa Mapitio ya Kipindi Maalum (UPR) Mhe. Katimba amesema kuwa Tanzania imeendelea kupiga hatua katika kukuza, kulinda na kuendeleza haki za binadamu kupitia utekelezaji wa mapendekezo ya kimataifa pamoja na juhudi za ndani za serikali. Ameeleza kuwa mafanikio hayo yamechangia kuimarisha amani, mshikamano na utulivu nchini, huku akisisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kulinda haki za msingi kwa kuzingatia sheria, sera na mikakati mbalimbali bila ubaguzi. Aidha, amebainisha kuwa Tanzania imekubali kutekeleza mapendekezo 187 yaliyotokana na ahadi ya kitaifa mbele ya jumuiya ya kimataifa, hatua inayolenga kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya taifa. Katimba amewahimiza wataalamu kuhakikisha wanaandaa taarifa yenye ubora na takwimu sahihi zinazoakisi hali halisi ya utekelezaji wa haki za binadamu.
back to up