Instagram story viewer> @tzembassyfr> Posts
2.1K
followers
69
following
Official Account for Tanzania Embassy in France
POSTS STORIES REELS TAGGED
TANZANIA YAIMARISHA UTANGAZAJI WA UTALII KATIKA SOKO LA UFARANSA NA ULAYA

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, kwa kushirikiana na Axium Collective, umeandaa hafla ya chakula cha mchana na majadiliano ya utalii tarehe 16 Oktoba 2026, jijini Paris, ikiwa ni hitimisho la Tanzania Leaders Club Roadshow 2026.

Hafla hiyo, iliyoongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Yakubu, imewakutanisha wawakilishi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Qatar Airways, Tanganyika na kampuni nyingine za utalii na hoteli. Pia imehudhuriwa na waandaaji wa safari na waandishi wa habari za utalii nchini Ufaransa, pamoja na baadhi ya washiriki kutoka Uholanzi, Ubelgiji na Luxembourg.

Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Yakubu ameeleza kuwa juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, zimeendelea kuimarisha utangazaji wa vivutio vya Tanzania kimataifa, ikiwemo kupitia filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

Amehimiza kuendelezwa kwa juhudi hizo kupitia kampeni za kidijitali kwa lugha ya Kifaransa, safari za utambulisho kwa waandishi wa habari na waandaaji wa safari, pamoja na kuimarisha ushirikiano na mashirika ya ndege ili kuongeza watalii kutoka Ufaransa na masoko mengine ya Ulaya.

Aidha, amewahamasisha wadau kuandaa vifurushi vinavyounganisha vivutio mbalimbali vya Tanzania Bara na Zanzibar, ili kuwapa wageni uzoefu mpana, kuongeza muda wa kukaa nchini na kupanua manufaa ya utalii kwa wananchi.

Balozi Yakubu ameishukuru Axium Collective, taasisi na kampuni zilizoshiriki pamoja na wadhamini kwa kufanikisha roadshow hiyo, akisisitiza umuhimu wa kugeuza mawasiliano yaliyojengwa kuwa ushirikiano wa kudumu na ongezeko la safari za watalii kwenda Tanzania. by @tzembassyfr
1
2 days ago
Download
TANZANIA NA UFARANSA ZAJADILI KUENDELEZA USHIRIKIANO BAADA YA MKUTANO WA AFRICA FORWARD

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Yakubu, amekutana na kufanya mazungumzo na Bi. Cassiopée Vienne, Naibu Mkurugenzi wa Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, katika Ofisi za Ubalozi jijini Paris.

Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa, hususan namna ya kuendeleza ushirikiano huo kufuatia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Africa Forward uliofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Kikao hicho kilitoa fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu vipaumbele vya nchi hizo mbili na namna ya kutumia fursa zinazotokana na Mkutano wa Africa Forward kuimarisha uhusiano na kuendeleza ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.

Ubalozi unaendelea kushirikiana na Serikali ya Ufaransa pamoja na wadau mbalimbali katika kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kufungua fursa za ushirikiano kwa manufaa ya Tanzania na wananchi wake. by @tzembassyfr
0
2 days ago
Download
RAIS MHE. DKT. MWINYI: USHIRIKIANO NA REAL MADRID FOUNDATION KUINUA VIPAJI VYA VIJANA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema ushirikiano kati ya Real Madrid Foundation na Unicorn Zanzibar Sports Limited utafungua fursa kwa vijana wa Zanzibar kukuza vipaji vya soka, kujenga nidhamu na kuimarisha maadili kupitia mafunzo yanayozingatia viwango vya kimataifa.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo , tarehe 13 Oktoba 2026, jijini Madrid, nchini Uhispania, wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano inayolenga kuanzisha programu maalumu za mafunzo ya soka kwa vijana, zitakazofuatwa na kuanzishwa kwa akademia ya kudumu katika Viwanja vya Michezo Zanzibar.

Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amepokea jezi ya timu ya Real Madrid kutoka kwa Roberto Carlos, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Balozi wa Real Madrid, pamoja na Julio González Ronco, Mkurugenzi wa Real Madrid Foundation. Tukio hilo limekuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika kukuza michezo na vipaji vya vijana Zanzibar na limehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa,Mhe Saidi Yakubu.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendeleza zaidi ya viwanja 30 vya mpira wa miguu na itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo, maarifa na mifumo itakayowawezesha vijana kufikia uwezo wao. Aidha, amesisitiza kuwa mafanikio katika michezo yanahitaji vipaji, nidhamu, elimu na makocha wenye ujuzi na weledi. by @tzembassyfr
0
2 days ago
Download
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mheshimiwa Saidi Othman Yakubu, akiwasilisha rasmi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa Emmanuel Macron, mjini Paris, katika Ikulu ya Élysée.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili maendeleo ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa, hususan katika sekta ya biashara inayoendelea kukua. Rais Macron pia alimpa Balozi Yakubu salamu za pole azifikishe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mumewe, Marehemu Hafidh Ameir.

@wizara_mambo_ya_nje_tz @owm_tz @msemajimkuuwaserikali @maelezonews @franceintanzania @mahmoudkombo @saidiyakubu1 @french_government @unesco_fr @af_dar by @tzembassyfr
0
13 days ago
Download
BALOZI YAKUBU AKUTANA NA MWENYEKITI WA BODI YA UTENDAJI YA UNESCO

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika UNESCO, Mhe. Saidi Yakubu, amekutana kwa mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya UNESCO, Dkt. Nasser Hamad Al Hinzab, jijini Paris, Ufaransa.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walibadilishana mawazo kuhusu namna ya kuendeleza michezo, utamaduni, elimu na sayansi kupitia mamlaka na programu za UNESCO. Walijadili pia umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi wanachama katika kuhakikisha shughuli za Shirika hilo zinakidhi mahitaji na vipaumbele vya maendeleo vya wananchi.

Bodi ya Utendaji ni chombo muhimu katika uongozi wa UNESCO, chenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano Mkuu, kutathmini programu na makadirio ya bajeti ya Shirika, pamoja na kufuatilia utekelezaji wake. Mwenyekiti wa Bodi ana nafasi muhimu ya kuongoza mijadala, kuratibu kazi za Bodi na kuwezesha nchi wanachama kufikia maelewano kuhusu masuala yanayohusu mwelekeo na utendaji wa UNESCO.

Mazungumzo hayo yalikuwa fursa kwa Balozi Yakubu kuelewa umuhimu wa kutumia majukwaa ya UNESCO kuendeleza vipaumbele vya Tanzania katika elimu, sayansi, utamaduni na michezo, pamoja na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika shughuli za Shirika hilo.

Dkt. Nasser, ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Qatar katika UNESCO, alimweleza Balozi Yakubu kuwa maandalizi ya Mkutano wa Bodi ya Utendaji unaotarajiwa kuanza Jumatatu yamekamilika. Mkutano huo utatoa nafasi kwa nchi wanachama kujadili masuala muhimu yanayohusu programu, usimamizi na utekelezaji wa majukumu ya UNESCO. by @tzembassyfr
0
15 days ago
Download
BALOZI WA TANZANIA ASHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA MWAKA WA ISO JIJINI PARIS

Paris, 28 Septemba 2026 — Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Othman Yakubu, ameungana na ujumbe wa Tanzania katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) unaofanyika jijini Paris. Ujumbe huo unaongozwa na Profesa Othman Chande, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Hafla ya ufunguzi imehutubiwa na Rais wa ISO, Dkt. Khaled Soufi, pamoja na Katibu Mkuu wa shirika hilo, Sergio Mujica. Mkutano wa mwaka huu, unaofanyika kuanzia tarehe 28 Septemba hadi 2 Oktoba 2026, umebeba kaulimbiu “Kujenga Imani katika Dunia Inayobadilika” na unawakutanisha viongozi na wataalamu wa viwango kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Ushiriki wa Tanzania unatoa fursa kwa TBS na wadau wengine kufuatilia mijadala kuhusu mchango wa viwango vya kimataifa katika ubora wa bidhaa na huduma, biashara, ubunifu na ushirikiano wa kimataifa. by @tzembassyfr
0
21 days ago
Download
𝐏𝐚𝐩𝐚 𝐧𝐚 𝐊𝐢𝐬𝐰𝐚𝐡𝐢𝐥𝐢…

Papa Leo XIV alipokaribishwa kwa Kiswahili na mtumishi wa Ubalozi wa Tanzania Ufaransa akajibu “Ahsante”

@wizara_mambo_ya_nje_tz @msemajimkuuwaserikali @mahmoudkombo @saidiyakubu1 @ofisi_ya_waziri_mkuu_kazi @unesco_fr @wizara_sanaatz @tbc_online by @tzembassyfr
0
24 days ago
Download
TANZANIA YASHIRIKI IFTM TOP RESA 2026 JIJINI PARIS

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Yakubu, ameshiriki katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Utalii ya IFTM Top Resa 2026, yaliyoanza tarehe 15 Septemba 2026, katika Ukumbi wa Porte de Versailles jijini Paris. Maonesho hayo yatahitimishwa Alhamisi, tarehe 17 Septemba 2026.

IFTM Top Resa ni miongoni mwa majukwaa makubwa zaidi ya biashara ya utalii barani Ulaya, yakileta pamoja zaidi ya wataalamu 32,000, chapa 1,650 na maeneo 177 ya utalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa umeratibu ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo, huku Kamisheni ya Utalii Zanzibar ikiratibu kampuni 15 za Kitanzania, zikiwemo hoteli, mashirika ya ndege, mawakala wa utalii na wadau wengine muhimu wa sekta hiyo.

Ushiriki wa Tanzania unatoa fursa ya kutangaza vivutio vya kipekee vya Tanzania Bara na Zanzibar, kufanya mikutano ya kibiashara, kujenga ushirikiano mpya na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka Ufaransa na masoko mengine ya Ulaya.

Maonesho hayo yanajikita katika utalii wa mapumziko na biashara, usafiri wa anga, huduma za hoteli, teknolojia, mikutano ya kimataifa pamoja na utalii endelevu. Foreign Tanzania WizarayaUtaliinaMamboyaKale Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿 

#TanzaniaUnforgettable #VisitTanzania #Zanzibar #IFTMTopResa2026 #TourismDiplomacy by @tzembassyfr
0
a month ago
Download
TANZANIA KIVUTIO MAONESHO YA CHAKULA PARIS

Tanzania leo, tarehe 10 Septemba 2026, imeshiriki katika Maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Chakula (Village International de la Gastronomie) yanayofanyika katika Viwanja vya Place de la Concorde jijini Paris, Ufaransa.

Maonesho hayo, yaliyofunguliwa rasmi na Meya wa Jiji la Paris, Mheshimiwa Emmanuel Grégoire, yamezikutanisha nchi 73 kwa lengo la kutangaza vyakula vya asili, urithi wa kiutamaduni na utalii wa mataifa mbalimbali duniani.

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Othman Yakubu, aliwaongoza Watumishi wa Ubalozi pamoja na Watanzania wanaoishi Paris kushiriki katika maonesho hayo, ambapo Banda la Tanzania lilikuwa miongoni mwa vivutio vikubwa kutokana na vyakula, bidhaa na utamaduni wa Kitanzania uliooneshwa.

Utalii wa chakula ni miongoni mwa vivutio muhimu nchini Ufaransa. Jiji la Paris pekee lina zaidi ya mikahawa 6,000 inayotoa ajira kwa maelfu ya watu, huku likipokea takribani wageni 300,000 kwa siku.

Akizungumza katika maonesho hayo, Balozi Yakubu alisema ushiriki wa Tanzania ni muhimu katika kutangaza utamaduni, vyakula na bidhaa za taifa, sambamba na kuitangaza Tanzania kama eneo la kipekee la utalii.

Aidha, aliahidi kuwa Tanzania itajiandaa kushiriki kwa ukubwa zaidi katika maonesho hayo mwaka ujao ili kuongeza fursa za kuitangaza nchi, kuvutia watalii na kufungua masoko mapya ya bidhaa za Kitanzania.

Maonesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 10 hadi 13 Septemba 2026. by @tzembassyfr
1
a month ago
Download
Tanzania welcomes international investors and global capital at today’s Friends of Africa Group meeting held at the OECD Headquarters in Paris, France. H.E. Ambassador Saidi Yakubu highlighted Tanzania’s strong economic growth, investment opportunities and Vision 2050 ambition of building. by @tzembassyfr
0
a month ago
Download
TANZANIA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI NA MITAJI YA KIMATAIFA

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Othman Yakubu, amewakaribisha wawekezaji na taasisi za fedha za kimataifa kutumia fursa pana za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania, hususan katika sekta za nishati, miundombinu na uzalishaji viwandani.

Mhe. Balozi Yakubu alitoa wito huo tarehe 9 Septemba 2026, jijini Paris, wakati akichangia katika Mkutano wa Kundi la Marafiki wa Afrika katika Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), uliojadili namna ya kuimarisha upatikanaji wa fedha na uwekezaji kwa ajili ya mageuzi ya uchumi wa Afrika.

Katika mchango wake, Mhe. Balozi alieleza kuwa uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa wastani wa asilimia 6, ukichagizwa na sera bora za uchumi na uwekezaji pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani bilioni 100 katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025.

Aidha, alieleza kuwa Tanzania imeanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja na taifa lenye ushindani, ubunifu, viwanda imara na matumizi endelevu ya rasilimali zake.

Mhe. Balozi Yakubu pia ameipongeza OECD kwa kuanzisha Jukwaa la Uwekezaji la Afrika kwa Njia ya Mtandao—Africa Virtual Investment Platform (AVIP)—litakalosaidia kuongeza uwazi wa taarifa, kuunganisha miradi na wawekezaji na kuhamasisha mitaji binafsi kuelekezwa katika miradi ya maendeleo barani Afrika. Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 za awali zinazoshiriki katika jukwaa hilo.

Alihitimisha kwa kutoa wito kwa OECD na washirika wa Afrika kuendelea kuimarisha ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, masoko ya mitaji na majukwaa ya taarifa ili fursa na uwezo mkubwa wa uwekezaji wa Tanzania na Afrika kwa ujumla uweze kutambulika na kutumiwa kikamilifu. by @tzembassyfr
0
a month ago
Download
 by @tzembassyfr
0
a month ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up