Instagram story viewer> @latra_tz> Posts
119.4K
followers
29
following
Ukurasa Rasmi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini - Official Account for Land Transport Regulatory Authority - ISO 9001 Certified
POSTS STORIES REELS TAGGED
 by @latra_tz
12
3 months ago
Download
 by @latra_tz
19
3 months ago
Download
 by @latra_tz
3
3 days ago
Download
 by @latra_tz
8
4 days ago
Download
 by @latra_tz
0
4 days ago
Download
LATRA YAKABIDHI VIFAA MOI, KILELE CHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, OKTOBA 9, 2026

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imekabidhi vifaa na mahitaji ya wagonjwa kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), jijini Dar es Salaam, Oktoba 9 2026, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja na kutekeleza shughuli za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na viti vya magurudumu, magongo ya kusaidia kutembea na mahitaji mengine ya kijamii vinavyolenga kusaidia wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo, hususan watoto na waathirika wa ajali za barabarani.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo, Dkt. Lemeri Mchome, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, ameishukuru Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya LATRA, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, CPA, Dkt. Habibu Suluo, kwa msaada huo ambao utachangia kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Kwa upande wake, Afisa Huduma kwa Wateja Mkuu LATRA, Bw. Augustus Fungo, amesema msaada huo unaonesha dhamira ya Mamlaka ya kuwajali wadau wake na kuchangia ustawi wa jamii, hususan kwa kusaidia wagonjwa wa ajali za barabarani.

Wiki ya Huduma kwa Wateja inaadhimishwa kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026, kwa kaulimbiu “Kufanya Zaidi ya Kinachotarajiwa” (The Extra Mile), inayosisitiza umuhimu wa
kuwahudumia wateja kwa uweledi, ufanisi, uadilifu na uwajibikaji ili kufikia na kuzidi matarajio yao. by @latra_tz
0
5 days ago
Download
 by @latra_tz
6
8 days ago
Download
WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2026: LATRA YAWAFIKIA WASAFIRISHAJI BUZA

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewafikia watoa huduma za usafiri wa mabasi ya mijini (daladala) Kata ya Buza, Dar es Salaam, kwa kutoa elimu kuhusu majukumu ya Mamlaka na kusikiliza changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma za usafiri kwa wananchi.

Elimu hiyo imetolewa Oktoba 7, 2026 na Bw. Augustus Fungo, Afisa Huduma kwa Wateja Mkuu LATRA, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, inayolenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu majukumu ya Mamlaka pamoja na njia mbalimbali za kuwasilisha changamoto zinazojitokeza katika sekta ya usafiri ardhini.

Katika kikao hicho, watoa huduma za usafiri wa daladala walipewa fursa ya kueleza changamoto na kero wanazokutana nazo wakati wa kutoa huduma kwa wananchi wa Kata ya Buza, huku LATRA ikipata nafasi ya kueleza hatua zinazoweza kuchukuliwa katika kushughulikia masuala hayo.

Aidha, kikao hicho kiliazimia kuimarisha ushirikiano kati ya LATRA, wadau wa usafirishaji, Jeshi la Polisi na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke katika kupanga na kutekeleza mikakati ya kushughulikia kero na changamoto zinazohusu huduma za usafiri katika eneo hilo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha changamoto zinazowakabili watoa huduma na watumiaji wa usafiri zinapatiwa ufumbuzi kwa ushirikiano wa wadau husika, sambamba na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Wiki ya Huduma kwa Wateja inaadhimishwa kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026, kwa kaulimbiu “Kufanya Zaidi ya Kinachotarajiwa” (The Extra Mile), inayosisitiza umuhimu wa
kuwahudumia wateja kwa uweledi, ufanisi, uadilifu na uwajibikaji ili kufikia na kuzidi matarajio yao. by @latra_tz
5
8 days ago
Download
 by @latra_tz
0
8 days ago
Download
 by @latra_tz
0
8 days ago
Download
LATRA YADHAMINI MOI MARATHON KWA VIFAA VYENYE THAMANI YA MILIONI 10

Na Gloria Lyatuu – MOI

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeunga mkono maandalizi ya MOI Marathon kwa kutoa ufadhili wa vifaa tiba na mahitaji ya usafi vyenye thamani ya Sh milioni 10. Mchango huo ni sehemu ya kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja na kutekeleza wajibu wa LATRA wa uwajibikaji kwa jamii.

Akikabidhi vifaa hivyo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Afisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa LATRA, Augustus Fungo, amesema mchango huo unalenga kuunga mkono juhudi za MOI katika kuwahudumia wagonjwa, huku ukionesha dhamira ya LATRA ya kushiriki katika shughuli zenye manufaa kwa jamii.

Fungo amesema LATRA imeona umuhimu wa kuunga mkono MOI Marathon kwa kuchangia mahitaji muhimu ya hospitali.

Amesisitiza kuwa wakati MOI ikihamasisha jamii kwa kaulimbiu ya “Vaa Helmet, Ubongo Hauna Spea,” LATRA inasisitiza ujumbe wa “Mguu Hauna Spea,” ili kuwakumbusha watumiaji wa barabara umuhimu wa kujikinga na ajali na kulinda viungo vyao.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Lemeri Mchome, ameishukuru Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya LATRA kwa kuchagua kuunga mkono mahitaji ya wagonjwa, akieleza kuwa msaada huo una thamani kubwa kwa wagonjwa wanaopata huduma katika mazingira magumu ya kiuchumi.

“Baadhi ya wagonjwa wanaofikishwa MOI huwa katika hali mbaya kiasi cha kutoweza kujitambua, huku wengine wakikabiliwa na changamoto za kifedha zinazowafanya washindwe kugharamia baadhi ya mahitaji muhimu wanapokuwa hospitalini na vifaa tiba vikiwemo  viti mwendo, ,” amesema Dkt. Mchome.

Dkt. Mchome ameeleza kuwa takribani asilimia 70 ya wagonjwa wanaopata huduma MOI wanahusishwa na majeraha yatokanayo na ajali za barabarani, hali inayoonesha umuhimu wa kuimarisha elimu ya usalama barabarani na kuzuia ajali zinazoweza kusababisha ulemavu au kupoteza maisha.

Kutokana na hali hiyo, amewataka watumiaji wa barabara kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani, kuepuka mwendo usio salama na tabia ya kuyapita magari mengine bila tahadhari, akisisitiza kuwa kinga ni muhimu  kuliko Tiba haswa katika kupunguza majeraha by @latra_tz
0
8 days ago
Download
 by @latra_tz
1
9 days ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up