Instagram story viewer> @mdaushupavu> Posts
12.5K
followers
6
following
@mdaushupavuawards, powered by @holysmile, is a platform dedicated to recognizing and celebrating the positive impact of outstanding stakeholders.
POSTS STORIES REELS TAGGED
πŸ”₯ HIGHLIGHTS | USIKU WA WADAU SHUPAVU – WESTERN ZONE 2026 πŸ†

Ilikuwa zaidi ya tuzo. Ilikuwa ni usiku wa HESHIMA, USHINDI, FURAHA na KUUNGANISHA WADAU! ✨

πŸ“ Mpanda, Katavi palikuwa kitovu cha historia pale wadau kutoka KIGOMA β€’ TABORA β€’ KATAVI walipokutana katika jukwaa moja kusherehekea watu, biashara, kampuni, taasisi, vipaji na viongozi wanaoleta matokeo chanya katika jamii.

πŸ† Tuzo na heshima
🀝 Networking
πŸ₯‚ Gala Experience
πŸ“Έ Red Carpet & Media
🎢 Burudani na shangwe
🌍 Biashara, utalii, ubunifu na maendeleo ya jamii

Hizi ni baadhi tu ya HIGHLIGHTS za usiku uliothibitisha kuwa Kanda ya Magharibi ina watu, vipaji na taasisi zinazostahili kuonekana na kuthaminiwa.

KIGOMA. TABORA. KATAVI.
MIKOA MITATU. JUKWAA MOJA. HESHIMA MOJA. πŸ†

πŸ“… 01 SEPTEMBER 2026
πŸ“ ST MATHIAS HOTEL – MPANDA, KATAVI
πŸŽ–οΈ Organized by HOLYSMILE taken in Katavi Region by @mdaushupavu
5
a month ago
Download
Wadau mbalimbali mkoani Kagera, wakiwemo vijana wabunifu, wajasiriamali na viongozi wa jamii, wamepata motisha kubwa kufuatia kushinda tuzo za Mdau Shupavu zilizotolewa na taasisi ya Holy Smile chini ya uongozi wa Mkurugenzi wake, Bwana Arnold Bweichum.

Akizungumza kuhusu lengo la tuzo hizo, Bwana Bweichum amesema, 

"Tuzo za Mdau Shupavu zinafanywa kutambua na kuenzi juhudi za wadau wanaojituma kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Hatua inayofuata ni kueneza tuzo hizi katika Kanda ya Ziwa, ikijumuisha mikoa yote sita ya kanda: Kagera, Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Mara, ili kuhamasisha wadau wengi zaidi."

Tuzo hizo zimewachochea wadau kuongeza bidii na ubunifu katika shughuli zao, huku zikiwa chachu ya mshikamano na ari ya kuendelea kutoa mchango chanya kwa jamii. Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa, amewapongeza washindi na kuwataka kutumia nafasi zao kuhamasisha maendeleo, maadili mema na mshikamano miongoni mwa jamii.

#sisiniholysmile #mdaushupavu #tuzo #awards #lakezone #KANDAYAZIWA #bweichum # by @mdaushupavu
37
10 months ago
Download
Mkurugenzi wa HolySmile Afafanua Mafanikio ya Hafla ya β€œUsiku wa Wadau Shupavu & Tuzo za Mdau Shupavu – Kanda ya Ziwa 2025”

Mwanza, Tanzania – Mkurugenzi wa Taasisi ya HolySmile, @bweichumjr , ameelezea kuridhishwa kwake na mafanikio ya hafla ya Usiku wa Wadau Shupavu & Tuzo za Mdau Shupavu – Kanda ya Ziwa 2025 iliyofanyika tarehe 16 Februari 2026 katika GoldCrest Hotel, Mwanza.

Akizungumza mbele ya wanahabari, Mkurugenzi amesema, β€œHafla hii ni kielelezo cha mshikamano wa kikanda na heshima kwa wadau wote wanaochangia maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kiutamaduni katika Kanda ya Ziwa. Tumewaunganisha wadau kutoka sekta za umma, binafsi, wajasiriamali na mashirika ya kiraia katika jukwaa moja, tukithamini mchango wao na kushirikiana katika miradi ya maendeleo.”

Mkurugenzi alibainisha kwamba tukio hili, lililoandaliwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo na BASATA kama mdau wa heshima, limefanikiwa kutoa:

Tuzo kwa wadau shupavu kutoka kila mkoa wa Kanda ya Ziwa, ikiwemo Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu, Mara, na Kagera.

Fursa za networking na mazungumzo kati ya wadau, makampuni, wajasiriamali, na viongozi wa serikali.

Burudani ya moja kwa moja, ngoma za kitamaduni, na vipengele vya sanaa vilivyopambanua tukio.

Mkurugenzi pia aliongeza, β€œTuzo za Mdau Shupavu sio tu heshima kwa fedha au jina, bali ni chombo cha kuhamasisha mshikamano, kuendeleza ujasiriamali, na kuonyesha mfano wa maendeleo chanya kwa jamii. Hafla kama hii inatupa fursa ya kushirikiana na wadau wengine na kuongeza motisha kwa wale wanaotoa mchango chanya katika kanda yetu.”

Taasisi ya HolySmile inasema itachukua mafanikio ya hafla hii kama msingi wa kupanua na kuimarisha tuzo na networking katika hafla zinazofuata, kwa lengo la kudumisha mshikamano wa kikanda na maendeleo endelevu. by @mdaushupavu
60
8 months ago
Download
πŸ†βœ¨ MWANAMKE SHUPAVU AWARDS 2026

**HESHIMA KWA MWANAMKE, THAMANI KWA MCHANGO WAKE!** πŸ‘‘

Tuzo si kipimo cha ukubwa wa mafanikio pekee, bali ni alama ya kutambua juhudi, uthubutu, ubunifu na mchango wa mtu katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.

🌟 **MAMA KAYONZA** ametambuliwa kupitia **MWANAMKE SHUPAVU AWARDS 2026** kwa mchango wake katika sekta ya huduma za biashara, kutambua ubora na weledi wake katika utoaji wa huduma.

Tunaamini kwamba **nyuma ya kila mwanamke shupavu kuna historia ya mapambano, maamuzi ya kishujaa na ndoto ambazo hakukubali zife.**

Kupitia jukwaa hili, tunaendelea kuthamini wanawake wanaothubutu, wanaojenga, wanaoongoza na kuwa sehemu ya maendeleo ya jamii.

**Hongera sana MAMA KAYONZA!** πŸ‘πŸ†

**HOLYSMILE**
*Tunatambua na kuthamini.*

#MwanamkeShupavuAwards2026 #HolySmile #WomenOfImpact #WomenEmpowerment #CelebratingExcellence ShupavuAwards by @mdaushupavu
0
a day ago
Download
One step at a time πŸ™ by @mdaushupavu
32
a day ago
Download
2025/2026 πŸ†
Best content creator mkoa wa mara 

Shukrani kwa Mungu kwa ushindi huu! Asanteni sana mashabiki, wazazi, waandaaji na kila mmoja aliyenipa support. πŸ™β€οΈ

Best Content Creator πŸ†πŸ”₯ Hii ni yetu sote
@musomabarbershop taken in Musoma Mara Tanzania by @mdaushupavu
35
14 days ago
Download
ASANTENI SANA MARA β€” MMETUPA HESHIMA KUBWA!

Kwa kweli maneno yanaweza yasitoshe kueleza namna tulivyopokelewa na kupewa heshima katika Mkoa wa Mara. ❀️

Asante sana Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime kwa kukubali mwaliko wetu na kuja kuwa sehemu ya Mdau Shupavu Awards & Dinner Gala – Mara 2026. Uwepo wako ulikuwa heshima kubwa sana kwetu.

πŸ™πŸΎ Asante DC Major Gowele
πŸ™πŸΎ Asante sana OCD Tarime
πŸ™πŸΎ Asante sana Bwana Mussa Jr
πŸ™πŸΎ Asanteni viongozi, wageni na Wadau Shupavu wote mliojitoa kuwa sehemu ya usiku huu mkubwa.

Mara mmetufundisha jambo moja β€” ukiheshimu jamii, jamii nayo inakupa heshima.

Sisi kama HOLYSMILE, hatuchukulii upendo huu kama jambo la kawaida. Tumeondoka na deni la kurudi tukiwa wakubwa zaidi, bora zaidi na tukiwa na mambo mengine makubwa zaidi. πŸ”₯

MARA, HII HAIKUWA MARA YA MWISHO β€” TUTAREJEA! πŸ€πŸΎπŸ†

Asanteni kwa kutuamini.
Asanteni kwa kutupokea.
Asanteni kwa kutupa heshima.

SISI NI HOLYSMILE.
JAMII INA NGUVU. πŸ’ͺ🏾

β€” Arnold Bweichum Jr
Mratibu Mkuu – Mdau Shupavu by @mdaushupavu
2
14 days ago
Download
Grateful. Honoured. Inspired. πŸ†

Being named Best Female Social Impact Influencer 2026 by @mdaushupavu is more than an award it is a reminder that impact matters.

To everyone who has supported, believed in me, encouraged, me and stood with me along this journey, thank you. This recognition belongs to you too. ❀️🫑

I receive this award with gratitude, but even more with renewed responsibility. Let this be the fuel to do more, serve more, and create greater impact.

The journey continuesπŸš€
More work. More impact. Greater purpose.

#GodOverEverything #pendomridafoundation #youthadvocate taken in † Dreams † by @mdaushupavu
75
16 days ago
Download
29 SEPTEMBA 2026 β€” MARA πŸ†

Asante kwa kuja @mrpoul_brand

β€œTuzo inaweza kukaa kabatini, lakini thamani yake halisi hukaa kwenye maisha ya watu uliowagusa.”

Tarehe 29 Septemba 2026 haikuwa tu siku ya kutoa tuzo; ilikuwa siku ya kutambua juhudi, kuunganisha watu na kufungua milango ya fursa mpya.

Kwa kila aliyeshiriki, aliyepiga kura, aliyefika, aliyetuunga mkono na aliyekuwa sehemu ya safari hii β€” asanteni sana.

Kwa washindi, hongereni. Kumbukeni, tuzo si mwisho wa safari; ni dhamana ya kufanya zaidi kwa jamii.

Kwa ambao hamkushinda, safari haijaishia hapa. Wakati mwingine kutoshinda leo ni maandalizi ya kurudi kesho ukiwa bora zaidi.

Tunajenga zaidi ya hafla.
Tunajenga watu, mahusiano, fursa na historia.

Maana mwisho wa yote, ukubwa wa jukwaa haupimwi kwa mwanga uliokuwa ukumbini, bali kwa mwanga unaobaki ndani ya watu baada ya taa kuzimwa.

β€” Arnold Bweichum Jr
Mratibu Mkuu – Mdau Shupavu
HOLYSMILE | JAMII INA NGUVU

TUJITAMBUE β€’ TUUNGANE β€’ TUJENGE ZAIDI. πŸ† by @mdaushupavu
1
16 days ago
Download
 by @mdaushupavu
3
17 days ago
Download
 by @mdaushupavu
3
17 days ago
Download
HIGHLIGHTS | MDAU SHUPAVU AWARDS & DINNER GALA – MARA 2026 | SEASON 2

Jana, 29 Septemba 2026, ilikuwa zaidi ya usiku wa tuzo β€” ilikuwa ni usiku wa heshima, mafanikio, fursa na konekisheni. πŸ₯‚πŸ”₯

πŸ“ BLUE SKY HALL – TARIME MJINI

Wadau kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara walikutana pamoja kusherehekea watu, biashara, taasisi na viongozi wa jamii wanaoendelea kuleta mchango chanya kupitia kazi zao.

πŸ† Tuzo zilikabidhiwa kwa washindi
🀝 Wadau walikutana na kujenga konekisheni
πŸ₯‚ Dinner & Networking
🎢 Burudani
πŸ“Έ Red Carpet Moments
✨ Special & Distinguished Recognition

Kila tuzo iliyotolewa ilikuwa na ujumbe mmoja mkubwa: kazi nzuri inapaswa kuonekana, kuthaminiwa na kupewa nafasi ya kukua.

Kutoka MARA β†’ KANDA YA ZIWA β†’ TAIFA πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Safari inaendelea. Hatua haikwami.

Asanteni sana wote mlioifanya MARA SEASON 2 kuwa usiku wa kukumbukwa. β€οΈπŸ†

SISI NI HOLYSMILE.
JAMII INA NGUVU.

TUJITAMBUE β€’ TUUNGANE β€’ TUJENGE ZAIDI

#MdauShupavu #Mara2026 #Season2 #HolySmile #Tarime AwardsAndDinnerGala JamiiInaNguvu taken in Tarime, Mara, Tanzania by @mdaushupavu
3
17 days ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up