Instagram story viewer> @morogorokwanza> Posts
15839
posts
16.2K
followers
7441
following
MOROGORO KWANZA
📰 Habari | Matukio | Matangazo
🌿 Utalii wa Uluguru & Udzungwa & Mikumi
📲 WhatsApp: 0628 534 041
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
🎉 KUMEKUCHAAAA!!! 💃🏻💃🏻💃🏻HOME SWEET HOME! 🏡🔥Morogoro, tupo tayari kwa burudani ya nguvu! Usikose kuwa sehemu ya tukio hili.🎟 Tiketi zinapatikana THE PALS LOUNGE.Usisubiri hadi dakika za mwisho—chukua tiketi yako mapema!📞 Kwa mawasiliano zaidi:☎️ 061 281 8442☎️ +255 68 322 2144Karibu tusherehekee pamoja! 🎶🔥@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro by @morogorokwanza
0
a day ago
Download
🎉 MOROGORO! JUMAMOSI HATUMWI MTOTO DUKANI! 💃🏻💃🏻Usikose burudani ya nguvu! 🔥🎟 Tiketi zinapatikana THE PALS LOUNGE.⚠️ Epuka foleni, chukua tiketi yako mapema!Viingilio:👧 Watoto – TSh 5,000🧑 Wakubwa – TSh 10,000Meza:🥇 GOLD – TSh 150,000🥈 VIP – TSh 300,000👑 VVIP – TSh 400,000📞 Kwa mawasiliano na kuhifadhi nafasi: 061 281 8442Karibu tusherehekee pamoja! Usichelewe—nafasi ni chache! 🔥🎶@_bistar by @morogorokwanza
0
a day ago
Download
TOFAUTI YA USHURU YAZUA SINTAFAHAMU SOKO LA MAWENZI.Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro, leo Julai 24, 2026, wamegoma kufungua biashara zao wakipinga kiwango cha kodi ya pango la vizimba pamoja na kile wanachodai kuwa ni utozaji usio sawa wa ushuru ikilinganishwa na Soko Kuu la Kingaru.Wafanyabiashara hao wanadai wanalipa kodi ya pango la vizimba ya Shilingi 20,000 kwa mwezi na wanaitaka Serikali kuipunguza hadi Shilingi 10,000. Aidha, wamesema pamoja na kulipa kiwango hicho, soko hilo bado lina miundombinu duni inayowafanya wateja wengi kushindwa kufika kufanya manunuzi.Baada ya mazungumzo kati ya wafanyabiashara na uongozi wa soko, imeelezwa kuwa majibu rasmi kuhusu malalamiko hayo yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumanne.Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, alifika katika soko hilo na kuahidi kuyafanyia kazi malalamiko ya wafanyabiashara hao. Kufuatia ahadi hiyo, wafanyabiashara walikubaliana kwa kauli moja kurejea na kuendelea na shughuli zao za biashara kama kawaida huku wakisubiri uamuzi wa uongozi.@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro by @morogorokwanza
0
a day ago
Download
AJALI YA MALORI MAWILI YASABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA MOROGORO.Malori mawili yamegongana uso kwa uso na kuwaka moto alfajiri ya leo, Julai 24, 2026, katika barabara kuu ya Morogoro–Iringa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori lililokuwa limebeba mchanga kuelekea Chalinze, ambaye aliacha njia na kugongana na lori lililokuwa limebeba kemikali aina ya Sulphur.Ajali hiyo imesababisha kifo cha mtu mmoja, mwanaume mtu mzima, huku watu wawili wakijeruhiwa na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.ACP Kantimbo amewataka watumiaji wote wa vyombo vya moto, hususan madereva wa malori ya masafa marefu, kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro #Morogoro #Ajali #UsalamaBarabarani #JeshiLaPolisi #Habari by @morogorokwanza
0
a day ago
Download
💦 KARIBU CHOMA WATERFALLS – ULUGURU MOUNTAINS, MOROGORO 🌿⛰️Tunawakaribisha wanafunzi, taasisi, vikundi, familia na wageni binafsi kutembelea Choma Waterfalls, kivutio cha kipekee kilichopo ndani ya Milima ya Uluguru.Njoo ufurahie matembezi ya asili, utalii, kujifunza kuhusu mazingira na uzuri wa mandhari ya milimani. 🌳💧Tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo:✅ Uongozi wa watalii (Tour Guide)✅ Ratiba za matembezi na utalii✅ Ushauri wa safari✅ Huduma kwa vikundi na wageni binafsi✅ Usafiri kutoka SGR hadi hotelini na kuendelea na safari za Choma WaterfallsKwa taarifa zaidi kuhusu mapokezi ya wageni, gharama na huduma zetu, tupigie au tutumie WhatsApp:📞 0628 534 041🌿 Choma Waterfalls Morogoro – sehemu sahihi ya kutalii, kujifunza na kufurahia uzuri wa asili.Karibu sana Choma Waterfalls by @morogorokwanza
0
2 days ago
Download
Kumekuchaaaa!!! 🤣🔥Mwenye Morogoro yake ni mkali hatari! 😂😂 Hii Jumamosi huyu lazima ashikiliwe kabisa, maana burudani itakuwa ya kiwango cha juu! 🎤🎉Morogoro, mpo tayari au bado? 👀🔥@dijavacompany @prince.jmmy @kunta_password @lamataleah @juakali_tamthilia @kombolela_season_2_official @azamtvtz @dijjahcollection_handbags @raskazone_classic @jambo_drinks @the_palstz @jovano_world @charlz_mmmh @morogoro_ndio_home @morogoroyetu @habarimorogoro @aboodmediatz @dizzimfm @planetfmtzHabari Morogoro – Sauti ya Morogoro. 🎙️❤️#Morogoro #KombolelaSeason2 #Burudani #HabariMorogoro #SautiYaMorogoro@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro @_bistar by @morogorokwanza
0
2 days ago
Download
GreenLeadership | Kijana Anayebadili Maisha Kupitia Kilimo na Mazingira 🌱Mkurugenzi wa Shirika la AgriWezesha Tanzania, Bibi Ignas Deograsia (@ignasdeograsia), ni mmoja wa viongozi vijana wanaotoa mchango mkubwa katika sekta ya kilimo na mazingira.Kupitia ushirikiano na Serikali ya Mkoa wa Morogoro, anaendelea kutekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuboresha maisha ya wananchi kupitia kilimo endelevu na uhifadhi wa mazingira.Kitaaluma ni Msimamizi wa Rasilimali Watu, lakini alifanya uamuzi wa kuacha ajira yenye mshahara mzuri na kujikita katika kujiajiri kwa kuanzisha AgriWezesha Tanzania (@agriwezeshatz), taasisi inayojihusisha na maendeleo ya kilimo na mazingira.Katika jukwaa la #VijanaUongoziForum, alipata fursa ya kushiriki uzoefu wake na kuelezea fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na mazingira (Green Opportunities), akihamasisha vijana kuona sekta hizo kama chanzo cha maendeleo na ajira.Hongera na ahsante, Bibi Ignas Deograsia, kwa mchango wako katika kuwainua vijana na jamii kupitia kilimo na mazingira. 🌿👏#GreenLeadership #VijanaUongoziForum #Kilimo #Mazingira Morogoro AgriWezesha Vijana@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro by @morogorokwanza
0
2 days ago
Download
Mguu wa kutoka Mora umebarikiwa! 🙏🏾✨Kwa wote wanaotoka Morogoro kwenda kutafuta riziki, Mungu awatangulie, awalinde na awabariki katika shughuli zenu za kila siku.Kama wewe ni mtafutaji wa kila siku, tukutane hapa kwa salamu. Mungu azidi kufungua milango ya mafanikio kwetu sote. 🤝#Watafutaji #Morogoro #Maisha #Baraka #SafariNjema@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro by @morogorokwanza
0
2 days ago
Download
Jeshi la Polisi Kilombero lakutana na wamiliki na madereva wa vyombo vya moto Ifakara kuimarisha usalama barabaraniJeshi la Polisi Wilaya ya Kilombero limekutana na wamiliki na madereva wa vyombo vya moto mjini Ifakara kwa lengo la kuimarisha usalama barabarani na kupunguza ajali kupitia utoaji wa elimu kuhusu sheria za usalama barabarani.Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kilombero (DTO), Blandina Kasongwa, amesema kila dereva wa chombo cha moto, ikiwemo trekta, anatakiwa kuwa na leseni halali ya Daraja G ili kuimarisha usalama barabarani na kuzingatia matakwa ya sheria.Aidha, DTO Blandina amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha madereva wanaowaajiri wanamiliki leseni halali ya Daraja G na wanatimiza masharti yote ya kisheria yanayohusu uendeshaji wa vyombo hivyo.@ikulu_mawasiliano @patrobasskatambi_ @wizara_ya_mambo_ya_ndani @rs_morogoro @dc.kilombero @polisi.tanzania @habarimorogoro :Sauti ya Morogoro #Kilombero #Ifakara #UsalamaBarabarani #JeshiLaPolisi #Morogoro by @morogorokwanza
0
2 days ago
Download
Hii ndiyo Habari Morogoro – Sauti ya Morogoro kwa sasa! 🎤🔥Morogoro imeanza kuhesabu saa kuelekea BISTAR NA MASHABIKI – SEASON 2: HOMECOMING FESTIVAL, itakayofanyika 25 Julai 2026 katika Pals Night Club & Lounge.Hamasa inaendelea kupamba moto kupitia Habari Morogoro na Bistar, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu usiku wa burudani ya kipekee.Sasa ni zamu yako! Kama wewe ni shabiki wa Kombolela, ni msanii gani kwenye orodha ya watakaotumbuiza ndiye atakayekufanya usikose kufika ukumbini au kufuatilia tukio hilo?Tuandikie jina lake kwenye maoni na utuambie kwa nini ndiye chaguo lako. 🔥👇#BistarNaMashabiki #HomecomingFestival #Morogoro #HabariMorogoro@_bistar@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro by @morogorokwanza
0
3 days ago
Download
Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa ya kifo chako. Umeacha simanzi kubwa mioyoni mwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote waliokufahamu.Mungu akujalie pumziko la milele na akuweke mahali pema peponi. Maisha yako yamekuwa funzo kubwa kwa wengi, na kumbukumbu zako zitaendelea kuishi mioyoni mwetu.Tunatoa pole za dhati kwa familia yako, hususan kwa kijana mwenzetu na Mkurugenzi wa @pii_media_tz, pamoja na ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huu.Mwenyezi Mungu awape nguvu, subira na faraja katika kipindi hiki kigumu.Pumzika kwa amani, Mzee wetu. Tutakukumbuka daima. 🤍🕊️@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro by @morogorokwanza
2
3 days ago
Download
📍 *Future Specialized Dental Clinic*_Kiliniki Bingwa ya Kinywa na Meno_Jengo la Equity Bank, Floor 03 – Morogoro Mjini📞 *+255 717 006 007*⏰ Jumatatu–Ijumaa: 8AM–11PM | Jumamosi: 8AM–2PM━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🏥 *Huduma ya Bima ya Afya kwa Huduma ya Kinywa na Meno Zinapatikana:*✅ NHIF | ✅ Jubilee Insurance━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━💚 *Karibu! – Daktari Yuko Wakati Wote!* by @morogorokwanza
0
3 days ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up