Instagram story viewer> @habarimorogoro> Post
3 days ago
Co Creator: morogorokwanza
0
Posted On: July 23rd 2026, 07:59 am
Tagged Users:
GreenLeadership | Kijana Anayebadili Maisha Kupitia Kilimo na Mazingira 🌱

Mkurugenzi wa Shirika la AgriWezesha Tanzania, Bibi Ignas Deograsia (@ignasdeograsia), ni mmoja wa viongozi vijana wanaotoa mchango mkubwa katika sekta ya kilimo na mazingira.

Kupitia ushirikiano na Serikali ya Mkoa wa Morogoro, anaendelea kutekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuboresha maisha ya wananchi kupitia kilimo endelevu na uhifadhi wa mazingira.

Kitaaluma ni Msimamizi wa Rasilimali Watu, lakini alifanya uamuzi wa kuacha ajira yenye mshahara mzuri na kujikita katika kujiajiri kwa kuanzisha AgriWezesha Tanzania (@agriwezeshatz), taasisi inayojihusisha na maendeleo ya kilimo na mazingira.

Katika jukwaa la #VijanaUongoziForum, alipata fursa ya kushiriki uzoefu wake na kuelezea fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na mazingira (Green Opportunities), akihamasisha vijana kuona sekta hizo kama chanzo cha maendeleo na ajira.

Hongera na ahsante, Bibi Ignas Deograsia, kwa mchango wako katika kuwainua vijana na jamii kupitia kilimo na mazingira. 🌿👏

#GreenLeadership #VijanaUongoziForum #Kilimo #Mazingira Morogoro AgriWezesha Vijana

@habarimorogoro :Sauti ya Morogoro

More posts

back to up