Posted On: July 25th 2026, 10:06 am
#HABARI Vijana Wilayani Tanganyika mkoani Katavi wametumia mikopo ya Halmashauri kufungua kampuni ya vifaa vya umeme ambayo imewawezesha kupata fursa za kufanya kazi na taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo TANESCO.
Hayo yameelezwa wakati Waziri wa Vijana, Joel Nanauka, akihitimisha ziara yake mkoani Katavi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, Kijiji cha Ilela, ambapo amewataka vijana kuchangamkia fursa za mikopo ili kujikwamua kiuchumi.
Waziri Nanauka amesema ameona namna halmashauri za mkoa huo zinavyotekeleza utoaji wa mikopo kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, huku wengi wakitumia fursa hiyo kuanzisha miradi mbalimbali.
Amesema vijana, wanawake na makundi maalumu mkoani Katavi wameonyesha mwitikio mzuri katika kutumia mikopo hiyo kuanzisha shughuli za uzalishaji na kuongeza kipato.
Katika ziara hiyo, Waziri Nanauka pia ametembelea miradi mbalimbali ya sekta za afya na elimu inayotekelezwa katika halmashauri za mkoa wa Katavi.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha