Instagram story viewer> @fr.johnassey> Tagged
POSTS STORIES REELS TAGGED
Kwa furaha na shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Mkurugenzi amempongeza Fr. Noel kwa mafanikio makubwa aliyoyapata kwa kuibuka miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo yake katika Chuo Kikuu nchini Italia.

Mafanikio haya ni ushuhuda wa bidii, nidhamu, maarifa na neema ya Mungu. Ni fahari kwa familia ya Mashirika ya Roho Mtakatifu na kwa jumuiya nzima ya Tengeru Boys na Holy Ghost Inclusive Secondary School.

Tunampongeza Fr. Noel kwa hatua hii muhimu ya kitaaluma na tunamwombea Mwenyezi Mungu azidi kumjalia afya, hekima na baraka nyingi ili aendelee kulitumikia Kanisa na jamii kwa uaminifu na ubora.

Hongera sana, Fr. Noel! Ad multos annos!
18
Tengeru Boys Secondary School & Holy Ghost Inclusive Secondary School extend their heartfelt best wishes to all our Form Four candidates as they begin their final examinations tomorrow.

May the Almighty God bless you with wisdom, knowledge, understanding, clarity of mind, a good memory, confidence, simplicity, integrity, and success throughout every examination. May His presence go before you, remain with you in every paper, and guide you safely from the beginning to the very end.

To all our parents, alumni, friends, and well-wishers, thank you for your unwavering support and prayers. Let us continue to stand united in prayer ifor our boys,our ambassadors as they represent our schools with excellence and dignity.

May the Almighty Lord hear your prayers, strengthen you, and crown your efforts with outstanding success.

Go with God. Excel with integrity. Return with victory
59
Tengeru Boys na Holy Ghost Inclusive High School tunawatakia kila la heri watahiniwa wetu wa Kidato cha Nne katika Mitihani ya Taifa.

Tunawaombea hekima, utulivu, afya njema na ujasiri. Mwenyezi Mungu awaongoze, awatangulie na awajalie mafanikio makubwa. Fanyeni kila mtihani kwa bidii, nidhamu na uaminifu.

Tunawaamini, tunawaombea na tunawatakia ushindi!

#TengeruBoys #
#holyghostviziwi_arushatz#
50
25
Wakati wa mahafali, baadhi ya wazazi walitoa Sadaka ya Shukrani kwa Mwenyezi Mungu wakimshukuru kwa neema zake nyingi alizowajalia wana wao katika kipindi chote cha miaka minne ya masomo katika Shule ya Sekondari Tengeru Boys. Walimshukuru Mungu kwa ulinzi, afya njema, hekima, mwongozo na mafanikio aliyowawezesha kuyafikia hadi kufikia hatua ya kuhitimu.

Kupitia sadaka hiyo, wazazi waliinua sala zao kwa Mwenyezi Mungu wakimwomba aendelee kuwabariki, kuwalinda na kuwaongoza wanafunzi hao wanapoelekea kufanya mitihani yao ya Taifa (NECTA), ili awajalie utulivu wa akili, hekima, afya njema na mafanikio makubwa katika mitihani yao na maisha yao ya baadaye.
11
10
30
Katika usaili wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza uliofanyika Tengeru Boys Secondary School, Meneja wa Shule, Fr. John Assey, aliwahamasisha wazazi pia kuzingatia nafasi zilizopo katika Marian Boys Secondary School pamoja na Shule za Holy Ghost Zanzibar, ambazo zote ni sehemu ya familia moja ya shule za Holy Ghost (Spiritan).

Shule hizi zinaendeshwa kwa misingi ile ile ya malezi bora, nidhamu, ubora wa taaluma na maadili ya Kikristo, zikitoa fursa zaidi kwa wazazi kuwapatia watoto wao elimu yenye ubora ndani ya familia moja ya kuaminika.

Chagua Shule za Holy Ghost leo, mjenge msingi imara wa kesho.

Ukijiunga na Familia ya Tengeru Boys, unabaki kuwa sehemu ya Familia ya Holy Ghost daima.
100
Ndoto huanzia na hatua ya kwanza. Leo, maelfu ya wanafunzi na wazazi wamefanya hatua hiyo kwa kuichagua Tengeru Boys Secondary School.

Kuanzia alfajiri, mazingira ya shule yalijaa hamasa, matumaini na ndoto za vijana waliowasili kutoka pembe mbalimbali za Tanzania kushiriki usaili wa kuomba nafasi za masomo. Kila mzazi aliyefika alikuwa na tumaini la kuona mtoto wake akipata elimu bora, malezi yenye maadili, nidhamu, uongozi na uwezo wa kujitegemea.

Mwitikio huu mkubwa unaendelea kuthibitisha imani ambayo jamii imekuwa nayo kwa Tengeru Boys Secondary School kwa miaka mingi. Ni heshima kubwa kwetu kuona wazazi na wanafunzi wengi wakichagua kuwa sehemu ya familia yetu.

Tunawashukuru kwa dhati wazazi, walezi na wanafunzi wote waliojitokeza leo. Tunawatakia kila mmoja mafanikio katika hatua hii muhimu ya safari yake ya elimu, na tunaahidi kuendelea kulea vijana wenye maarifa, maadili, uzalendo na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Karibu Tengeru Boys Secondary School — mahali ndoto zinapoandaliwa kuwa mafanikio.

Once a Tengeru Boy, Always a Tengeru Boy. 💙

Tengeru Boys Secondary School
*Education for Self Reliance. *
128
back to up