Instagram story viewer> @raykhan_tz> Tagged
3.5K
followers
1994
following
🎵 Music • Entertainment • Lifestyle
👑 Creating. Inspiring. Evolving.
🇹🇿 Tanzania
📩 Business/Collabs ↓
POSTS STORIES REELS TAGGED
Asante sana mdogo wangu @raykhan_tz kwa zawadi yangu Wow wow wow hii Nyimbo level Bravo @raykhan_tz
14
Ninashukuru Salvation Army kwa kunitunuku tuzo hii ya heshima na ya kipekee.

Sijioni @miriamodemba kuwa bora kuliko wengine, la Hasha. Najiona ni mwanamke mwenye deni la kurudisha kwa jamii inayonipenda kwa dhati, jamii ya watu wanaoishi katika uhitaji, na makundi maalum.

Hii ni jamii ya watu wenye moyo kama wangu, ndoto kama zangu, na furaha kama yangu. Wanacheka, wana hisia, wana imani, na pia wana uthubutu, kama wangu, tenaa wanaishi kama mimi..

Kuwa mlemavu haizuii kufanikiwa, haizuii kuwa na furaha, wala haizuii kubidiika. Maana kipimo cha vyote hivi hakipo kwenye mwili wala machoni, bali ndani ya nafsi zetu na mioyo yetu sote.

Ahsanteni sana na Mungu awabariki. Thanks my Team. @miriam_odemba_foundation  Videographer @msangi.images  Music by @raykhan_tz  @jacktzee  Team yangu Asanteni sana : @jennifer_fred_mteleke  @rimaly_syd_odemba @charliimedia  @sautiyamitindo  @directorkinny_  @studio__kitaa  @ms_.janeth  @jestinakalage
15
Nimelia Sana kwa Furaha Asante Mungu kwa hii Tuzo 🙏🏿🫶🏿 @miriam_odemba_foundation Nawashukuru sana kwa kuja.

Nimekuwa mwanzilishi wa  Miriam Odemba Foundation ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii. 

Taasisi yetu imejenga shule, madarasa, visima, na pia kushiriki moja kwa moja katika kugusa maisha ya mwanamke, watoto na hasa mabinti katika jamii.

Tumehudumia mabinti katika kampeni zetu mbalimbali za kufanikisha ndoto kwa wengi, ikiwemo kwenye kuinua elimu, kuinua vipaji, kufundisha maadili, na kuhamaasisha maendeleo ya afya ya mwili na akili.

Tangu taasisi kuanzishwa, imekuwa njia ya kufanya kazi mbalimbali za kijamii, huku ikishuhudia jinsi mwanzilishi wa taasisi hii akipenda kucheza na watoto, kucheka nao na kuwahudumia katika mahitaji mbalimbali.

Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, au maarufu kwa jina la Matumaini;  Salvation army imekuwa kituo mama kwa Miriam Odemba kila ninapokuwa nyumbani, iwe likizo au kwenye majukumu mengine, nimekuwa ,nikiwatembelea watoto karibia kila mwaka.

Furaha hii ya Miriam Odemba kusherehekea siku ya kuzaliwa ni ishara ya upendo wa dhati kwa jamii nzima ya kitanzania hasa wale wenye uhitaji, ikiwemo walio kwenye makundi maalum.

Furaha yangu ni kuona watoto wanakula, wanavaa, wanacheza na hata kujifunza, ili waendelee kuamini katika ndoto zao, malengo, na kujiamini katika maisha na ukuaji.

Leo ninatimiza miongo zaidi ya minne duniani, na bado naishi na kuamini katika utu, fadhili, maadili na kuzingatia malezi bora, hata wasioweza kuyapata.

Nawapenda wote, na ninatamani kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wenzangu kuwa na moyo kama wangu na zaidi, na naamini, hii inatujenga kuwa na jamii bora, kuliko zote, zenye utu, asili na hadhi halisi ya kiafrika.

Ahsanteni sana, nawapenda wote.

Miriam Odemba Foundation, changing the future of Tanzania.  Thank you Team : @jennifer_fred_mteleke  @charliimedia @rimaly_syd_odemba @raykhan_tz  @ms_.janeth  @studio__kitaa  @sautiyamitindo @msangi.images  @_isher_official  @ateta_dahylan @abdul.tilla
22
back to up