Instagram story viewer> @feints.live> Tagged
23.9K
followers
21
following
All about Sports📌
Founded by @rich.kizza10
Subscribe official YT channel - Feints Live
[email protected]; for anything
POSTS STORIES REELS TAGGED
1.Simba wamefanikiwa kukusanya alama tatu lakini wanapaswa kuboresha sana kwenye eneo la ushambuliaji kwasababu leo ndani ya kipindi cha kwanza Simba walikuwa hawana utulivu pamoja na umakini kwenye matumizi ya nafasi 

2.Fountain Gate ni timu dhaifu mno hasa wakiwa hawana mpira kuna muda hawaelewi nini wanapaswa kufanya hawajui muda gani,kwa namna gani na wapi wanatakiwa kufanya pressing wala hawafahamu watumie mbinu ipi kuzuia je wanapaswa kukaba mtu kwa mtu (man to man defending) au kukaba nafasi (zonal defending) kiufupi hali ni mbaya sana 

3.Anicet Oura na Libasse Gueye ni specialist hasa pale unapowahitaji kutengeneza hatari kuanzia mbele ya safu ya ulinzi ya timu pinzani kutokana na ubora kiufundi,kasi na maarifa waliokuwa nayo mfano rejea goli la Libasse leo pamoja na goli la Anicet dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo uliopita 

4.Kocha wa Simba hakuwa na mashaka kumtumia Kante kama single pivot kutokana na udhaifu wa Fountain Gate,moja kati ya changamoto kubwa kwa Kante ni kujua na kuwadhibiti wachezaji wanaofanya sana movements bila ya mpira kutokea katikati ya kiwanja lakini pia hana uwezo wa kukaba eneo kubwa la uwanja usisahau ni mchezaji ana ufundi wa hali ya juu sana anapokuwa na mpira mguuni maana yake uwezo wake kuanzisha au kuendeleza mashambulizi ni wa daraja la juu sana 

5.Toure na Rushine wana kitu kimoja ambacho nimeona wanafanana ambapo wote wanaweza kuanzisha na kuendeleza mashambulizi kwa kupasia na kusafiri na mpira licha yakuwa leo FG walikuwa wanawapa nafasi na muda wa kutosha naendelea kumtazama zaidi 

NB:

1.Kibabage anafanya sana movements bila ya mpira anahitaji kuwa na muendelezo kwenye utoaji wa huduma kwa washambuliaji ila nishati,kasi na upambanaji ✅

2.Minziro kachukua kibarua kigumu mno 😄

3.Chama ni tafsiri na maana ya mchezaji mwenye uelewa wa mpira 

4.Napenda mentallity na matamanio ya Mpanzu kwasasa kila akipata dakika anaonyesha matanio ya kutaka kushinda
12
Angalia mpaka mwisho😀
59
back to up