Instagram story viewer> @millardayo> Posts
88022
posts
15.7M
followers
1503
following
Award winning TV/Radio Personality | Amplifaya @cloudsfmtz |Journalist from Africa | Bookings [email protected] | 📍 DSM, Tanzania
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Najua kwa sasa habari ya Mjini ni Katoro, Geita lakini kwa Wawekezaji wajanja siku zote huangalia zaidi fursa zilizopo Zinga Bagamoyo kuliko kelele za Mjini.

Kwa wanaojua thamani ya uwekezaji wa mapema, mwelekeo wetu ni Zinga, Bagamoyo Mkoani Pwani kwenye eneo la zaidi ya ekari 300 zilizotengwa kwa uwekezaji ulio salama, wenye kufikika kirahisi na uliozungukwa na huduma muhimu za kijamii.

Zinga kuna Viwanja vya Viwanda vinavyoanzia mita za mraba 5,000 pamoja na Viwanja vya Makazi vya mita za mraba 600, vinavyofaa kwa kuishi au kuwekeza kwa manufaa ya baadaye.

Moja ya sifa kubwa za eneo hili ni ukaribu wake na Jiji la Dar es salaam pamoja na kuzungukwa na huduma muhimu za kijamii kama maji, umeme, hospitali na shule, hali inayolifanya kuwa eneo bora kwa uwekezaji wa muda mrefu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na timu yetu kupitia 0703 100 100.
#MillardAyoUPDATES by @millardayo
726
10 days ago
Download
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche amewataka Mawakili wa chama hicho kujiandaa kwa ajili ya kuhakikisha wanawasaidia kutoka Viongozi wa chama hicho waliokamatwa.

Heche ameyasema hayo leo Julai 25, 2026 Jijini Mwanza mbele ya Waandishi wa Habari, akisisitiza kuwa CHADEMA itapambana kwa nguvu zote kuhakikisha Viongozi wake wanaoshikiliwa katika maeneo mbalimbali wanaachiwa huru na kurejea kuungana na familia zao.

“Hata makande tutakula ili watoke,” amesema Heche.
#MillardAyoUPDATES by @millardayo
445
an hour ago
Download
Celebrate the Queens of Football! ⚽👑 From 26 July to 16 August, follow the action of the @totalenergies_tz TotalEnergies CAF Women’s Africa Cup of Nations Morocco 2026. Visit your nearest TotalEnergies service station to learn more and celebrate the passion of women’s football with us.

 #TotalEnergiesCAFWAFCON2026 #FootballTogether by @millardayo
15
2 hours ago
Download
Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa hii leo Julai 25, 2026 amemtembelea na kumjulia hali mdau wa muziki na mlezi wa vipaji nchini, Mkubwa Fella, nyumbani kwake kwa lengo la kumjulia hali, ambapo pia amemkabidhi msaada wa shilingi milioni 20.

Katika ziara hiyo, Majaliwa alipata nafasi ya kufanya mazoezi mepesi ya viungo pamoja na Mkubwa Fella, ikiwa ni sehemu ya kumpa moyo katika kipindi hiki cha kuendelea kuimarisha afya yake.

Aidha, wawili hao walifanya mazungumzo kuhusu mchango wa Mkubwa Fella katika kukuza na kuendeleza muziki wa Tanzania, hususan katika kulea na kuinua vipaji vya Wasanii mbalimbali, pamoja na masuala mengine yanayohusu maendeleo ya tasnia ya sanaa Nchini.
#MillardAyoUPDATES by @millardayo
343
2 hours ago
Download
Usisubiri siku ziishe bado una nafasi ya kuwasilisha wazo bunifu litakaloweza kubadili mfumo wa ukusanyaji kodi Nchini huku likikuweka kwenye nafasi ya kujishindia hadi TSh milioni 50 kwani zimebaki siku sita pekee kabla TRA haijafunga rasmi dirisha la kupokea mawazo.

Kupitia Innovation Portal inayopatikana kwenye tovuti ya TRA kila Mtanzania anaalikwa kushiriki kwa kuwasilisha wazo litakalosaidia kupunguza changamoto za ulipaji kodi kurahisisha matumizi ya Akili Mnemba AI katika ukusanyaji wa kodi pamoja na kubuni njia rahisi zitakazorahisisha huduma kwa Walipakodi

Kumbuka dirisha la kupokea mawazo bunifu linafungwa Julai 31 2026 hivyo usikubali fursa hii ikupite tuma wazo lako sasa na uwe miongoni mwa washindi 1,020 watakaozawadiwa huku ukichangia mageuzi ya mfumo wa kodi Nchini. #MillardAyoUPDATES by @millardayo
118
3 hours ago
Download
JIZOLEEEEEEEE kwa hadi 80%

Badilisha muonekano wa nyumba yako kwa gharama nafuu! 

Pata hadi 80% OFF kwenye fanicha na bidhaa mbalimbali za Cash & Carry @gsmhometz.
📍 GSM Plaza, Kamata pekee.
📞 +255 792 377 377
#SaleSaleSale #Punguzo #GSMHomeTZ by @millardayo
20
5 hours ago
Download
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa leo Julai 25, 2026 katika Uwanja wa Mnara wa Mashujaa, Dodoma.

Mbali ya Rais Samia, Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni miongoni mwa Viongozi waliokuwepo.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Julai 25 kwa lengo la kuwaenzi mashujaa waliopoteza maisha wakitetea, wakipigania na kulinda uhuru, amani na maslahi ya Taifa la Tanzania.

Katika maadhimisho hayo, shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo dua na sala maalum za kuwaombea mashujaa waliotangulia mbele ya haki pamoja na kuliombea Taifa liendelee kuwa na amani na mshikamano. 
#MillardAyoUPDATES by @millardayo
653
5 hours ago
Download
Hatua ya mwisho kabla ya pambano kubwa imekamilika baada ya bondia wa Mafia Boxing Promotion, Asemahle Wellem kumaliza rasmi zoezi la Faceoff kuelekea pambano la kuwania mkanda wa dunia wa IBO World Light Heavyweight.

Wellem atapanda ulingoni kesho, Julai 25, 2026, Nchini Kazakhstan kumkabili bondia wa nyumbani Ali Akhmedov katika pambano linalotarajiwa kuvuta hisia za Mashabiki wa ndondi duniani.

Mbali na kuwa bondia wa Mafia Boxing Promotion, Wellem pia ni Balozi namba moja wa Kombe Real Estate, huku akiiwakilisha Tanzania na Afrika katika harakati za kutafuta ubingwa wa dunia.
#MillardAyoUPDATES by @millardayo
77
17 hours ago
Download
Hali ya taharuki imeibuka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure leo Julai 24, 2026 baada ya Ndugu wa marehemu Wambura Mambiya (54) kuingia kwenye mgogoro wa kugombea mwili wake, huku kila upande ukitaka kuwa na mamlaka ya kuamua mahali atakapozikwa.

Mgogoro huo ulianza baada ya Mke Mkubwa wa marehemu, Elizabeth Nyakao kudai kupata taarifa kuwa baadhi ya Ndugu wa marehemu walikuwa wakipanga kuuchukua mwili na kuupeleka kwa siri kwa ajili ya mazishi bila kuwashirikisha. 

Elizabeth amesema aliishi na marehemu kwa miaka 32 kabla ya kutengana naye takribani miaka mitano iliyopita.

Kwa upande wake, Binti mkubwa wa marehemu, Happiness Wambura amesema yeye pamoja na Wanafamilia wengine walifika hospitalini ili kuhakikisha mwili hauchukuliwi bila makubaliano ya familia.

Akizungumza kwa niaba ya familia, kaka wa marehemu Gladson Mambiya amesema chanzo cha mgogoro huo ni marehemu kuacha wake wawili, huku akidai kuwa kabla ya kufariki aliwahi kueleza kuwa alitamani azikwe kwa Mke Mdogo.

Hata hivyo, baada ya mvutano huo, familia imefikia uamuzi wa kuupeleka mwili wa marehemu Musoma kwa ajili ya mazishi, hatua inayolenga kumaliza mgogoro na kuzuia mivutano zaidi kati ya pande zinazohusika.
#MillardAyoUPDATES by @millardayo
743
20 hours ago
Download
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ametangaza vita dhidi ya madanguro na vitendo vya ukiukwaji wa maadili, akisisitiza kuwa Serikali haitamvumilia Mtu yeyote anayejihusisha na biashara hizo au kuwatumia Watoto katika vitendo vya unyanyasaji.

Akizungumza na Wananchi Jijini Dar es salaam, Mpogolo amelipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua za haraka walizochukua kuwakamata Watuhumiwa wa vitendo hivyo, akisema operesheni hizo zimezuia madhara zaidi kwa Jamii.

Amesema taarifa zinaonyesha kuwa katika Kata ya Zingiziwa kulikuwa na Mtu anayeshukiwa kuwatumia Watoto wa Kike kuwachezesha wakiwa hawana nguo kwa malipo ya kati ya shilingi 3,000 na 5,000 ambapo Mtuhumiwa amekamatwa na uchunguzi unaendelea.

“Niwapongeze sana Jeshi la Polisi kwa umakini wao wamechukua hatua mapema kabla madhara hayajaongezeka, ushahidi uliopo utawezesha Sheria kuchukua mkondo wake,” amesema Mpogolo.

Aidha, amewataka Wenyeviti wa Mitaa na Wananchi kushirikiana na Vyombo vya Dola ili kutokomeza madanguro, akisisitiza kuwa umaskini hauwezi kuwa sababu ya kuwahusisha Watoto au Wanawake katika vitendo vinavyodhalilisha utu.
#MillardAyoUPDATES by @millardayo
341
21 hours ago
Download
Kwa mabasi yanayopiga masafa marefu, tumia kilainishi cha Rubia chenye ubora na ufanisi wa hali ya juu.

Rubia ndio suluhisho la biashara yako karibu @totalenergies_tz 

#RubiaNdioSuluhisho  #totalenergiestz by @millardayo
15
a day ago
Download
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya (@dalmiamikaya) amewataka Wananchi wa Kigamboni kujenga utamaduni wa kufanya usafi wa mara kwa mara huku akipiga marufuku ujenzi holela wa madampo na utupaji takataka hovyo.

Dalmia ameyasema hayo leo Julai 24,2026 katika ziara yake ya Kampeni ya kuhamasisha usafi wa mazingira katika maeneo ya biashara na makazi Magogoni katika Kata ya Tungi.

“Nawasititiza Wananchi wa Kigamboni kuhakikisha kila mmoja kwenye eneo lake anafanya usafi, leo tumepita maeneo kadhaa mfano Kata ya Tungi, Kibada na Somangila tumeona Watu wanatupa taka hovyo maeneo sio rasmi, kuna maeneo wanatumia taka kutengeneza maeneo ya madampo,”

“Kuna Watu wanajenga work shop bila kufuata utaratibu kwenye maeneo yasiyo rasmi, tunataka Kigamboni iwe kwenye mpangilio safi, sio kujenga makazi na maeneo ya biashara holela, wito wangu pia usafi uwe wa mara kwa mara na mifereji isafishwe kwa wakati pia Wakandarasi wakusanye taka kwa wakati,”amesema Dalmia.
#MillardAyoUPDATES by @millardayo
48
a day ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up