Instagram story viewer> @call_for_env_conservation> Post
14 days ago
Co Creator: upendomwakyusa_
26
Posted On: October 21st 2026, 05:58 am
Tagged Users:
Wanawake 70 wanaojishughulisha na uokotaji taka Dodoma Mjini wanatarajiwa kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali wa kijani yatakayowawezesha kuongeza thamani ya taka wanazokusanya, kukuza kipato na kujipatia fursa endelevu za kiuchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na masuala ya Mazingira- Call for Environmental Conservation (CFEC), Upendo Mwakyusa, ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mafunzo hayo yatajikita katika kuwawezesha wanawake hao kutumia taka kama rasilimali inayoweza kuzalisha bidhaa zenye thamani zaidi.

Mwakyusa amesema kuwa mbali na ujasiriamali wa kijani na uongezaji thamani wa taka, wanawake hao pia watapatiwa ujuzi wa kutafuta masoko na kuboresha mbinu za kuuza taka wanazokusanya ili kuongeza tija katika shughuli zao ambapo kupitia mradi huo, shirika hilo linalenga kuwajengea wanawake uwezo wa kujitegemea kiuchumi kwa kutumia fursa zinazotokana na ukusanyaji na urejelezaji wa taka.

Mbali na hayo pia wanawake hao watapatiwa mafunzo ya afya na usalama mahali pa kazi pamoja na vifaa kinga, vikiwemo buti, glovu, barakoa, kofia za kujikinga na jua na jaketi zenye viakisi mwanga, kwa lengo la kupunguza hatari wanazokabiliana nazo wanapokusanya taka.

Aidha utekelezaji wa programu hiyo utafanyika kwa kushirikiana na mitandao ya wakusanyaji taka pamoja na wadau wengine wa eneo husika ili kuhakikisha wanawake wanaostahili wanapata fursa ya kushiriki na kunufaika na mafunzo hayo.
Comments (26)
ww3gifty_swai_tyre_seller 6 days ago

ww3gifty_swai_tyre_seller

Congratulations Boss🔥

lynne_jack99 9 days ago

lynne_jack99

My sissy uwiii🔥🔥🔥

sarah_marambo 11 days ago

sarah_marambo

🔥👏Goo dear

eng.luamba 13 days ago

eng.luamba

Proud of you

kaka_patrick_ 13 days ago

kaka_patrick_

@upendomwakyusa_ am proud of u 🙌🔥🔥🔥

fridaamaniofficial 13 days ago

fridaamaniofficial

🔥🔥🔥naam

sally_mosha 13 days ago

sally_mosha

👏👏👏😍

ayl42910 13 days ago

ayl42910

Proud of you madam 🔥

rebecca_manoti 13 days ago

rebecca_manoti

Proud of you @upendomwakyusa_ 👏

the_madame13 13 days ago

the_madame13

Proud of you my friend 😍😍😍

ted_bakedpleasures 14 days ago
_nsia 14 days ago

_nsia

👏👏👏👏

Load More

More posts

back to up