Instagram story viewer> @amrisaly> Posts
POSTS STORIES REELS TAGGED
Kuna njia mbili za kufikia mafanikio, 

Mwaka 2019 wakati naanza mchakato wa kutafuta kutafuta pesa nilikua na option ya kuchagua njia pia, 

1. Njia ya kwanza ni njia ya kufikia mafanikio taratibu (building wealth slowly), 
2. ⁠Njia ya pili ni njia ya kufikia mafanikio kwa haraka (building wealth fast), 

Kama ilivyo kwa kila mtu, nilichagua njia ya kwanza, 

nilikuwa  21 yrs, damu inachemka vibaya mno, vitu vingi navitamani sina namna ya kuvipata so there is no any way nichague njia ya kwanza, 

Nilishaingia kwenye ponze scheme, adstera, nimeshanunua Fx indicators, nishampa mtu acc anifanye management, nimeshakuwa hyped nikaingia kulima tikiti, nilikuwa nikisikia naweza kupata pesa faster chapu nipo, 

Kitu ambacho huwa najipongeza nacho ni; nipo faster sana kufanya maamuzi pale ambapo nimekosea njia, 

Na nikijua ukweli nipo faster sana kukubaliana nao, 

Sometimes inaumiza kufahamu kwamba; 

- Ku-build wealth slowly inachukua averagely miaka 15, 
- ⁠Lakini ku-build wealth faster inachukua averagely miaka 25, 

Hiyo miaka 10 yote ni ya kujifunza, kuzuia tamaa, manipulations, unrealistic expectation na kutambua kwamba there is no fast way to build wealth, 

Miaka 25 inaonekana mingi lakini  nimeongea na watu wengi ambao wanasema “after all these 25 years ndo nimegundua nilikuwa naenda kwenye njia isio sahihi”

Na ili ujue sio mingi, unawajua watu wangapi wapo 40 - 60+ yrs, ambao hawajaweza ku-build wealth na wameanza kupambana at their 20s, 

Kuna sababu nyingi lakini kuchagua njia ambayo sio sahihi ni sababu main,

Listen; Kuna trends nyingi zinaendelea na nyingine hata umeshaingia, 

Naweka wazi; ukisikia mtu anakuambia 1 - 2 yrs utatengeneza 500M,  Bilioni, etc na huna hata historia ya hata kupitisha 50M kwenye mikono yako nitakuambia kitu kimoja RUUUUN, 

Bila kujali huyo mtu anafanya biashara gani, ni nani wako, ana pesa kiasi gani,  hata kama ni mimi siku nikija kukuambia hivyo KIMBIA, tena usigeuke nyuma;

Ni bora mtu akueleze kabisa you can make lkn inahitaji miaka,

Nothing is IMPOSSIBLE but things take skills, discipline, dedication and most important TIME.

📍@intelligencefloor
📸 @baraka_photography 
🕴️ @mtani_bespoke 
👞 @gents_tools taken in Masaki by @amrisaly
133
8 months ago
Download
Nikitaka nisimkwaze wala kum-dissapoint mtu yoyote au kwa lugha rahisi nimfurahishe kila mtu inabidi nitenge at least laki 5 mpaka 1M kwa siku, 

Then nitenge minimum masaa sita kila siku, ku-chart na kuzungumza na watu even useless topics,

Lakini maisha hayapo hivyo,

Na sio mimi tu, hata wewe;

Inatakiwa ujiweke wewe kuwa number 1 priority, 

Na sometimes watu wanaweza kukuona m-binafsi na pesa zako, attention yako, muda wako, 

Lakini huo sio ubinafsi ni self respect and self love, 

Asilimia 99 ya watu unaofanya vitu ili kuwafurahisha, unaacha kufanya maamuzi sahihi ya maisha yako ukiwaza;

 “watanionaje”🤔

siku ukianguka, ukishindwa kufika malengo yako au kumudu mahitaji yako watakucheka alafu watasema “mimi nilijua tuu”

na kuna watu wengine utashindwa kuwaambia “NO” lakini just a year from now hawatokuwa kwenye maisha yako na tayari watakuwa wamekuchelewesha au wamekuharibia, 

Kama vile shule au chuo tu, unashindwa kuwa na msimamo wa kusema “NO” na kufocus na masomo, kujenga new skills,  unaenda na marafiki huku na kule, mnatoroka na kufanya vitu ambavyo havina mchango wowote kwako, hao marafiki mara ya mwisho hata kuongea nao lini?

Alafu the issue ni kwamba kama wewe unataka ku-ridhisha watu sababu ya kuwaza watakuonaje you can’t satisfy a person all the time, utajipinda leo, kesho, kesho kutwa ila ipo siku utashindwa kum-satisfy kwenye jambo fulani na yote ya nyuma hayato-make sense kwake,

Warren Buffet ana msemo wake mmoja anasema “The difference between successful people and really successful people is that really successful people say no to almost everything.”

Hii tabia ya kushindwa kusema no, kuset your standards na kuwaza watu watakuonaje, watakuwaziaje huwa ni developing behavior, as days goes inazidi kukutawala, 

- Utaogopa kumfukuza mfanyakazi wako anaezingua ukiwaza atanionaje biashara itakufa
- Utaogopa kumuacha mpenzi miyeyusho utakufelisha alafu atakuacha yeye
- ⁠Utaogopa kusema hapana kwenye kulinda pesa yako, utafirisika
- ⁠Utawaza watu wataonaje nikisema hapana ili kulinda muda wangu, utafika miaka 30, 40 au hata 60 huja-archive chochote

If you say yes to others, make sure you are not saying no to yourself. by @amrisaly
102
a year ago
Download
Ukipata pesa ghafla zinaisha, mshahara haukutani na mshahara mwingine, boom linaishi kwanza week tatu tu, huwezi ku-save, huwezi ku accumulate capital”, 

Unaweza kwenda mbali hadi kusema kuna chuma ulete au ukawa convinced kirahisi kwamba kuna nguvu za giza ambazo hazitaki wafanikiwe au kuna wachawi wanakuzuia, 

Mchawi kweli yupo ndio maana hupigi hatua kwenye maisha, jina lake ni “your new normal” 

Regardless unapata pesa nyingi au kidogo kiasi gani “your new normal” atakushika shati na kukurudisha nyuma, 

Miaka michache tu ulikuwa upo sawa kutumia infinix ila leo bila iphone ya mwaka wa mbele unahisi kuumwa,!

Ulikuwa unapanda daladala na unafika unapoenda fresh ila leo bila bolt hutoki, 

Kushusha kioo cha gari kununua kitu cha 10k kilicho nje ya budget yako kwako ni kawaida, 

Unapiga hesabu za kununua gari na hela hata ambayo hujaishika bado au hata unaingia kwenye madeni ili ununue gari, 

Chips chuku za 7500 kwako kawaida, unaona kupika huna muda na kunachosha,

Ulikuwa huwezi hata ku-afford kulipia miezi sita chumba cha elfu sabini bila kukopa, leo kukaa nyumba ya robo ya mshahara wako it’s normal,

Instead ya kuzoea kiwango kipya cha uwekezaji unazoea cha matumizi, 

Unapata pesa nyingi kuliko zamani ila kitu pekee unafanikiwa ni kuendesha maisha na kubaki na mfuko mtupu,

Inafika hatua maisha lazima tu yabadilike sababu utakuwa unafanya kazi kwa bidii, unatafuta pesa ili nini? 

Ila tatizo kubwa ni speed ya kutoka maisha uliyokuwa nayo mpaka kufika kwenye your new normal life,

Sikuambii haya ili uishi kwa kujitesa, mimi mwenyewe ndio maisha yangu, siku zote nachora mstari kati ya my normal life and my new normal, 

mimi mpaka leo sijioni nikihitaji 17 pro max, hata hii 16 nimenunua baada ya kutumia 14 for 3 years na kusumbua 🪫,

Nimekaa the same house for more than 5 years bila kuwaza kuhama pamoja na kipato kukua zaidi ya 10X, 

Nimekaa na zaidi 100M bank ila nilikua sina gari, mpaka hata nafungua trading floor ya kwanza pale skycity sina hata ist,

Sio kwa sababu nilikuwa sina uwezo wa kufanya hayo yote lakini ni kwa sababu najua principal ya weath ni 3M, 

Make money 
Manage money 
Multiply money

Na sio make money, use money, repeat taken in Masaki by @amrisaly
360
3 months ago
Download
“Either wewe ni mwizi au umerithi otherwise ni ngumu kupata pesa ukiwa kijana” hiki ndio kitu kilichopo kwenye akili za wengi, 

Ukweli unaoumiza ni kwamba pesa haina urafiki, undugu wala uhusiano na ujana au uzee

na watu wengi hawatofikia level ya kuwa financially free hata wakipewa nafasi ya kuishi 100 yrs, 

na sababu sio kutokuwa na pesa(mtaji) au kukosa muda wa kufanyia kazi melengo,

Bali kutokana na tabia mbaya chache, ambazo nimezi-experience kwa macho yangu, sio kwa kusimuliwa wala kusoma kwenye vitabu na sio kwa mtu mmoja au wawili,

Kufika stage ambayo pesa unayoingiza bila kufanya chochote ni kubwa kuliko matumizi yako, stage itakayofanya uamue ufanye kazi gani, saa ngapi na kuwa na full control ya maisha yako ukiwa na hizi tabia ni haiwezekani, ukizi-fix kila kitu kinabadilika,

1. Kupuuza roadmap; hakuna ambae hajui kupata pesa inahitaji kuwa na maarifa, descipline, kuanza biashara, kufanya kazi kwa bidii, kuitathimini kila leo umeitendea haki kiasi gani, wote tunajua mafanikio hayahitaji kuendekeza ulevi, ngono, betting, kubweteka,etc

2. ⁠Kuongea na kupanga sana na sio kuanza; vitu unavyosema utaanza kufanya tangu January mpaka leo tuu ungekuwa umeanza tayari ungekuwa sehemu tofauti na ulipo leo, na tatizo ni kutaka everything to be perfect ndio uanze na kutaka kuanza vitu ambavyo huna what it takes,

3. ⁠Kukaa kwenye mazingira ambayo sio sahihi na kuzungukwa na watu ambao sio sahihi;  badala ya kukimbizana kutafuta watu unaona ni sahihi, build value and your potential first, wewe uwe mtu sahihi kwanza,

4. Kufanya kazi kwa bidii lakini kwenye vitu, biashara, au kazi ambavyo sio sahihi, sehemu ambazo hata ukifanya kazi kwa bidii kiasi gani malipo hayawezi ku-grow exponentially

Bila hivi vitu, utaaminishwa na utaamini kwamba unatakiwa uwe mwizi, at the end uoga wa kufa masikini unaweza kukufanya ufe kijana au uishie jela, 

au uishi kwa kuamini one day yes, Mungu atajalia, wakati Mwenyezi Mungu ameshaweka principles za maisha kuwa ukifanya xyz utapata matokeo gani, 

nimeshakuwa kwenye stage ya kukosa buku mfukoni so naelewa mambo ni magumu lakini impossible is nothing and it’s never too late to start 💯

📸 @baraka_photography by @amrisaly
364
2 years ago
Download
It’s been a while since we posted something personal here… but today deserves it🤍

Happy Birthday to an incredible woman🎂

This year is even more special because I now get to celebrate you not only as the amazing person I love, but also as a beautiful mother, 

Watching you step into motherhood has been one of the most special things to witness, 

May this new year of your life bring you more joy, more love, and many more beautiful moments for our family❤️

9 years of memories… and the best chapters are still ahead.

📸 @baraka_photography by @amrisaly
357
7 months ago
Download
At 20 yrs old nilikuwa sina hata 100k kwenye bank account yangu, 

At 23 yrs old nilikuwa na zaidi ya 100M, 

At 27 yrs old nimeona zaidi ya 1B kwenye account yangu, 

Sitaki kuku-motivate, nataka nikuambie kitu kimoja na ukikielewa ume-win maisha, 

Hiki kinaamua mafanikio yako bila kujali una umri gani:

“Relationship yako na UNCERTAINTY”

Hicho kitu pekee kinaweza kukupeleka kwenye utajiri au kukuacha kwenye umasikini, 

hakuna njia yoyote maisha yatakwenda according to plan kila siku, kuna siku changamoto ambazo hujawahi kuzitarajia zitatokea, 

Hakuna binadamu hapitii changamoto zinazoweza kumuangusha, 

Maisha ni kama financial markets - Kwenye growth kuna Higher High (HH) na Higher Low (HL), 

Kwenye deterioration kuna Lower Low (LL) na Lower High (LH), 

Na kukutana na Stop Loss ni lazima, 

Kwa lugha isiyo ya ki-trading: Safari ya mafanikio haiwezi kuwa straight line, 

una-grow, halafu kitu kinatokea cha kukurudisha nyuma,  Kazi kubwa sio kuepuka changamoto - ni kuhakikisha tunazikabili na haturuhusu zibadili direction yetu ya maisha na kutoka kwenye series za Higher High na kuanza series za Lower Low, 

Changamoto sio adui ni chachu ya kupambana,

Personally nimepitia, bado napitia na kadri ninavyozidi kukua, natarajia kupitia changamoto kubwa zaidi, 

hakuna mwenye kinga ya changamoto lkn kuna watu ambao wamejiandaa kupigana na kushinda kila changamoto itakayokuja mbele yao, 

Tupo mwanzo wa mwaka, una very big plans,lakini kwenye plan yako hakikisha things not going according to plan is part of your plan, 

“Everyone has a plan until they get punched in the face.” ni  kweli lakini maumivu hayakuwa makali, na hayaji na mshtuko kama kupigwa tayari ni sehemu ya plan yako, 

Plan sio kushambulia tu,  plan pia ni kuwa defensive: kuwaza“Nikipigwa na maisha 3–0, game plan yangu itakuwa ipi?”

Supplier atazingua, partner atakusnich, mzigo utapotea, wezi watakuja, boss atakugeuka, cashflow itabadilika, mtaji utapukutika, etc

Hakuna mchakato wa kufika juu ulio rahisi, 

Ukiuona mchakato wako ni rahisi, jiulize kama kweli unaelekea juu, 

Kama unapitia magumu that’s how it’s supposed to be, 

Na kama hupitii magumu ipo siku utapitia, 

That is how life is. taken in Masaki by @amrisaly
301
9 months ago
Download
Masaa machache yamebaki kuelekea kwenye event yetu na kila kitu kiko tayari, ila bado kuna kitu kimoja nimekuwa nikifikiria tangu asubuhi

Siku 45 zilizopita wengi wetu hatukujuana kabisa, wengine walikuwa online wengine physically, kila mtu akiwa na sababu yake ya kuja. Kuna aliyekuja kwa sababu amechoka kupoteza pesa, kuna aliyekuja kwa sababu anataka kubadilisha maisha ya familia yake, na kuna aliyekuja kwa sababu tu alikuwa anatafuta watu wanaomuelewa

Tukapitia Beginners, Technical, Psychology, Propfirm masterclass mpaka Stock & Personal Finance, na kwenye hiyo safari tukajifunza kitu ambacho hakiko kwenye course yoyote. Trading ukiwa peke yako ni ngumu sana, ila ukiwa na watu wanaokuelewa, wanaokuuliza umetrade nini leo na wanaokushika mkono ukikosea, inakuwa safari tofauti kabisa

Ndiyo maana huwa tunasema lone wolf anaweza kushinda trade moja ila pack inashinda mwaka mzima

“Talent wins games, but teamwork and intelligence win championships.”

Kesho tunakutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza baada ya hizo siku 45, kwenye the most premium experience tuliyowahi kuandaa kwa ajili ya IFX 2026/27 Bootcamp members pekee. Mazingira ni mazuri lakini kitu kikubwa zaidi ni watu utakaokutana nao, connections utakazojenga na mazungumzo ambayo yanaweza kukufungulia milango usiyoitarajia

Kama umekuwa ukifuatilia safari yetu kwa mbali na ukatamani kuwa sehemu yake, huu ndio muda wako. Ukijiunga na bootcamp leo, kesho utakuwa pamoja nasi badala ya kuona picha online baadaye

tuwasiliane sasa

📲 WhatsApp: 0625 554 222 by @amrisaly
26
a day ago
Download
Siku 45 zilizopita, tulianza bootcamp kama strangers wengine online wengine physically 

Wengine hawakujua hata candle ni nini. Wengine walikuwa wameshaunguza account zaidi ya mara moja. Wengine walikuja kimya kimya, wakiwa wamechoka kujaribu peke yao.

Usiku baada ya usiku, tulikaa pamoja.
Beginners course. Technical course. Psychology course. Propfirm masterclass. Stock & Personal Finance.

Kulikuwa  na siku nzito zenye maswali mengi na maswali yaliyoamsha watu saa nane usiku. Lakini hakuna aliyepitia hayo peke yake.

Na kitu ambacho wengi kwenye trading hawakijui strategy inaweza kufundishwa na mtu yeyote. Kinachoifanya IntelligenceFX kuwa tofauti si chart, ni watu. Ni ile hali ya kujua kuna mtu atakushika mkono siku utakapotaka kukata tamaa.

“Talent wins games, but teamwork and intelligence win championships.”

Lone wolf anaweza kushinda trade moja Pack inashinda mwaka mzima ndiyo maana sisi hatushindi kwa bahati. Tunashinda kwa consistency.

Ijumaa hii, kwa mara ya kwanza baada ya siku 45, tunakutana uso kwa uso hii si event ya kawaida tumeandaa the most premium experience ever kwa ajili ya IFX 2026/27 Bootcamp members pekee. Mazingira ni ya hadhi, lakini thamani halisi iko kwenye chumba chenyewe: watu utakaokutana nao, connections utakazojenga, na mazungumzo yanayoweza kubadilisha mwelekeo wa maisha yako.

Mlango huu hautafunguliwa kwa kila mtu ni kwa wale walioamua na habari njema ni kwamba bado kuna nafasi.
Ukijiunga na bootcamp sasa, Ijumaa hii utapata nafasi ya kuattend kwenye hii event Hutakuwa ukiangalia picha zetu online  ukijiuliza “ingekuwaje kama ningekuwepo?”

📲 WhatsApp: 0625 554 222 by @amrisaly
86
a day ago
Download
Kama upo positive kuna vitu vingi sana utajifunza kutoka kwangu, 

Kama upo negative kuna vitu vingi sana kutoka kwangu vitakukera, 

Kamwe huwezi kuwa katikati,

Kuna wakati nimetoka chuo sina pakukaa nilienda kuishi kwa jamaa yangu anaitwa @bigdaddy_solo, nimesoma nae advance, nimeenda nae Jkt pia, alikuwa anasoma pale Sauti, 

Sauti wakafunga chuo, Solo akawa anarudi home, nikawa sina pa kwenda na siwezi kubaki hostel chuo kimefungwa, 

Kurudi nyumbani kwangu haikuwa option kabisa sababu nilikuwa nataka nipate sehemu ya kutulia nifocus na kujifunza, ku- practice na kufanya trading bila kuwa na any kind of distraction, 

Solo akaniambia “kuna jamaa yangu nasoma nae yeye amepanga nje ya chuo na haondoki kwenda likizo sababu ana biashara” 

Ndo alienda kuniombea kwa mtaalamu hapa niliyepo nae hapa kwenye picha @official_lixtz , pamoja na kwamba ilikuwa hatufahamiani jamaa alikubali nikaenda kuishi kwake,

Enzi hizo nilikuwa na ka-laptop kangu kamoja kabovu jamaa ananiacha nakodoa macho kwenye candlestick huku nikiwa naandika kwenye journal ya counter book yeye anaenda kupiga picha na kuuza t-shirt,

Sometimes nilikuwa nabaki sina shilingi ila ilikuwa tunapika na tunakula, bila shida wala manyanyaso yoyote, 

Nilijifunza vitu vingi sana huu wakati, 

Washkaji kama Lix wapo wachache sana kwenye hii dunia ya sasa, 

Ntaendelea kuku appreciate leo, kesho na siku zote🫡

kijana yeyote aliye serious kutafuta mafanikio, hasa kupitia financial markets, ni lazima awe na uelewa mpana wa uchumi, finance, financial markets na global economic events

Kujua technical analysis pekee haitoshi, unatakiwa kuelewa pia nguvu zinazoendesha markets, historia ya financial crises, monetary policy, inflation, interest rates na jinsi maamuzi ya kiuchumi duniani yanavyoathiri masoko ya fedha

anza kwa kujifunza kuhusu matukio haya muhimu katika historia ya uchumi na financial markets

1. Great Depression (1929–1939)
2. 1970s Inflation and Oil Crisis
3. Black Monday (1987)
4. Asian Financial Crisis (1997–1998)
5. Dot-com Bubble (1995–2002)
6. Global Financial Crisis (2007–2009)
7. European Sovereign Debt Crisis (2010–2012)
8. Swiss Franc Shock (2015)
9. COVID-19 Market Crash (2020)
10. Glo by @amrisaly
2k
3 days ago
Download
it’s not about money, ni kuhusu kupeana motisha, kushare powerful trading ideas na kujenga team yenye uwezo wa kufanya kazi pamoja, ku-execute with confidence, ku-journal trades na kudumisha discipline 🔥

unatamani kuona analysis na review ya trades zilizofanyika recently na traders wetu pale kwenye trading floor? 👀

kaa karibu na YouTube channel ya IntelligenceFx this week, leo tunaanza na video namba 1, na tuna mengi ya ku-share kutoka kwenye trading floor

📺 leo saa 21:00, YouTube ya IntelligenceFx

don’t miss this one 🔥 by @amrisaly
36
4 days ago
Download
Hii ndiyo highlight ya bila filta yetu ya mwisho kuachiwa, 

lakini tayari kuna nyingine jikoni, tumesha-record na kwa sasa inapikwa vizuri, and trust me, this time it’s going to be very different 👀

kwa mara ya kwanza kabisa, bila filta tunakuja na girl guest wamoto sana,

keep enjoying this one as we prepare to serve you another masterpiece,

1. Kitu gani umekipenda au umekichukia kutoka kwenye episode hii ya bila filta?,

2. Unadhani ni nani huyo msichana atakayekuwa mgeni wetu kwenye bila filta inayofuata?, 

drop your guesses in the comments and stay tuned👇

Real conversation | Different perspectives taken in Dar es Salaam, Tanzania by @amrisaly
170
5 days ago
Download
Nimeishi, nimekutana, nimeongea na watu ambao ni very successful,

Nimefanya kazi na biashara na watu ambao ni very successfully, 

Pia nimeishi na watu ambao ni maskini na hata mimi umasikini nimeuishi, 

Na kitu kimoja ambacho natamani kila kijana ajue ni kwamba;

1. Sio kwamba watu waliofanikiwa wana akili sana, wapo smart sana au ni watu exceptional❌,

Wanaofanikiwa ni ni watu ambao ambao wapo faster kwenye kufanya maamuzi, kusimamia maamuzi yao, ku-take calculated risk, kujifunza kutokana na makosa, wanafanya kazi kwa bidii, wanafeli sana kuliko watu masikini sababu wanafanya sana vitu na hakuna kitu watu masikini wanaogopa kama ku fail, 

2. Na kitu kikubwa zaidi ni wana-THINK BIGGER✅, 

Na ku-think bigger sio mara zote kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria, 

Ni kuwa na mindset ya -  matter what, no matter nitakuwa kwenye changamoto kubwa kiasi gani, no matter nitakuwa na ufinyu wa resources kiasi gani lakini lazima kuna njia ya kufanya  ili kufika malengo, 

Huku watu masikini wanafikiria zaidi kitu kinachowazuia kufanya vitu vya kuwapeleka kwenye mafanikio na kujiaminisha kwamba hakuna njia na kujipa limitation,

Na it’s very hard kubadili hiyo hali, very very hard, 

Kwanza ni ngumu hata tu mtu kujua kwamba ana hali kama hiyo na ndo inamzuia kufanikiwa, 

The simplest way ya kujibadilisha ni kuji-expose kwenye mazingira ya watu wanaofanya vitu consistently na kufanikiwa, 

Na ugumu wa hii njia ni kwamba watu ambao wanafanya vitu consistently hawapendi kujichanganya na watu ambao ni energy drainers au ambao kila kitu wanaona ni kigumu na hakiwezekani,

Hivyo you have to commit yourself to change, ukubali kubadilika, kusikiliza, kujifunza na uonyeshe kweli upo tayari kwa mabadiliko before hujaanza kuji-associate na watu hao,

Na it’s very hard kubadili hiyo hali, very very hard, 

Kwanza ni ngumu hata tu mtu kujua kwamba ana hali kama hiyo na ndo inamzuia kufanikiwa, 

Just think ni hali ambayo umedumu nayo tangu umezaliwa, probably kwa miaka 20 to 45+, unadhani kitu ulichokiishi miaka yote ni itakuwa rahisi kubadili? Sio rahisi Lakini inawezekana💯

How? Soma full kwenye instagram story ya @amrisaly, kuandika yote kwenye caption haitoshi. by @amrisaly
74
7 days ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up