Unakumbuka ulivyojisikia ulipomaliza Kidato cha Nne?
Kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pwaga, ambao ni wanachama wa Klabu ya CDF, kuhitimu Kidato cha Nne ni hatua muhimu inayofungua ukurasa mpya wa maisha yao.
CDF tulipata fursa ya kuwatembelea, kuwapongeza kwa hatua hii muhimu na kuwatia moyo wanapojiandaa kuanza safari nyingine ya elimu na maisha kwa ujumla.
Tulipata pia nafasi ya kutafakari pamoja kuhusu mambo waliyojifunza kupitia klabu hizi, ikiwemo kujiamini, kutambua haki zao, kufanya maamuzi sahihi na kushiriki katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Tuliahidiana kuendelea kuwasiliana na kufuatilia maendeleo yao hata baada ya kumaliza shule, kwa sababu safari yao ya kujifunza na kukua inaendelea.